Mambo
makubwa yamefanyika katika uwanja wa CCM Kirumba usiku huu jijini
Mwanza ambapo Mwanamuziki Gwiji Barani Afrika kutoka Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo Kofii Olomide amepagawisha mashabiki wa muziki
wake, katika tamasha la Tusker Carnival na kukonga nyoyo za mashabiki
wa muziki jijini humo, Mwanamuziki Kofii Olomide akiwa na kundi lake
amefanya kilichokuwa kikitarajiwa pamoja na hamu ya mashabiki kupiga
kelele kwa madai ya kutaka kumuona mwanamuziki huyo mahiri barani
Afrika.
Kofii Olomide amefanya mambo
makubwa kama alivyoshusha burudani jana kwenye viwanja vya Leaders
jijini Dar es salaam, Watu mbalimbali wamiminika kwenye uwanja wa CCM
Kirumba ili kumuona mwanamuziki huyo pichani juu akiwa na mwimbaji wake
anayejulikana kwa jina la Cindy akimtambulisha kwa mashabiki wa jijini
Mwanza .
Kamanda wa Fullshangblog
alikuwepo jijini Mwanza ili kukumuvuzishia moja kwa moja matukio hayo
usiku huu kutoka katika uwanja wa CCM Kirumba Kaa mkao wa kuperuzi mara
kwa mara katika ukurasa wa Fullshangwelog ili kujua kinachojiri uwanjani
hapo .
|
No comments:
Post a Comment