Monday, December 24, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ATEMBELEA NA KUWAJULIA HALI WAZEE WA MKOKOTONI-MKOA WA KASKAZINI UNGUJA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na mkewe Mama Asha Bilal, wakitoka ndani kwa Haji Machanu, Mbalungini Mkoa wa Kaskazini Unguja, wakati walipokuwa katika ziara ya kuwatembelea wazee kwa ajili ya kuwajulia hali, leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishiriki kuomba dua na Mzee Juma Muhidin Mohamed, Mkazi wa Mkokotoni Shangani Mkoa wa Kaskazini Unguja, wakati alipomtembelea kumjulia hali wakati akiwa katika ziara yake ya kuwatembelea wazee kwa ajili ya kuwajulia hali, leo. Mzee huyo anasumbuliwa na ugonjwa wa miguu. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na mkewe Mama Asha Bilal, wakizungumza na Mzee Maalim, Sheha Haji Machame, Mkazi wa Mkokotoni Shangani Mkoa wa Kaskazini Unguja, wakati walipokuwa katika ziara ya kuwatembelea wazee kwa ajili ya kuwajulia hali, leo.Mzee huyo anasumbuliwa na ugonjwa wa kuuma kwa miguu.
Picha Zote na OMR

No comments:

Post a Comment