
Mwanamuziki wa Kizazi Kipya Rehema
Chalamila maarufu kama RAY C jana amemtembelea Rais Dkt.Jakaya Mrisho
Kikwete ikulu jijini Dare s Salaam na kumshukuru kwa msaada wa matibabu
wakati alipokuwa mgonjwa hivi karibuni.Rehema aliyefuatana na Mama yake
Mzazi Margareth Mtweve na Dada yake Sarah Mtweve alimweleza Rais kuwa
afya yake imeimarika na kwamba muda si mrefu atarejea jukwaani kukonga
nyoyo za mashabiki wake.Kwa apande wake ,Mama Mzazi wa Ray C amemshukuru
Rais Kikwete kwa kuokoa maisha ya mwanaye na vilevile ametoa wito kwa
watu wanaokusanya michango kwaajili ya mwanaye waache kufanya hivyo
kwani matibabu ya Ray C yamegharamiwa na Rais.

No comments:
Post a Comment