Monday, January 28, 2013

CHADEMA WA AHIDI KULIVALIA NJUGA SWALA LA GESI, PIA WAUKATAA MUUNGANO WA KULAZIMISHA

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Mh Freeman Mbowe akizungumza katika kikao cha Dharura cha Kamati kuu ya CHADEMA ya kujadili Mustakabali wa chama hicho kwa kipindi hichi ambapo wanakaribia kwenye Uchaguzi.
 Katika Hotuba yake Mh Mboqw amesema kuwa miongoni mwa mambo ambayo wanatarajia kuyashughulikia kipindi cha kutafuta uongozi wa kushika Dola ni kuhakikisha kuwa Katiba mpya itakayopatikana itakuwa inajali Maslahi ya Umma na kama sivyo watawashawishi Umma kuikataa katiba hiyo kwani wanaiamini nguvu ya Umma.

Mh Mbowe amesema kuwa, kwa Kanda ili kila kuwepo na maamuzi katika kila kanda ambapo kuna kanda kumi na zitahakikisha kuwa mchakato wa kuin'goa Serikali iliyopo Madarakani unaanzia sasa kwa kasi mpaka siku ya kupiga kura.

Amezungumzia pia Swala zima la Gesi na kuitaka Serikali kutatua kwa kusikiliza matatizo ya wakazi wa Mtwara ili Gesi hiyo iwanufaishe tena kwa haraka na kuongeza kuwa wanalivalia Njuga swala la Gesi ya Mtwara kuhakikisha kuwa wakazi wa Mtwara wanafaidika na Gesi yao kwa makubaliano mazuri ya Serikali.

Mh Mbowe amesema pia katika Swala zima la Gesi ya Mtwara wanahitaji mikataba yote 26 iwekwe wazi kwani kuficha au kuifanya siri ni Dalili ya kutaka kuwatapeli watanzania.

Amezungumzia pia swala la Muungano na kusema kuwa Zanzibar waachiwe nchi yao na Watanganyika wadai Tanganyika yao kwani katika Katiba ya Zanzibar tayari  hawaukubali Muungano.

"Muungano tunautaka lakini hatutaki muungano wa kulazimisha ni afadhali kila mtu akabaki na serikali yake watanganyika na Serikali yao na Wazanzibar na Serikali yao"amesema Mbowe.
Mwenyekiti Mbowe pamoja na Viongozi wengine wa CHADEMA wakipunga Bendera za chama hicho
Katika Mkutano huo CHADEMA ilifanikiwa kumnasa aliyekuwa naibu katibu mkuu wa chama cha NCCR MAGEUZI Bw, Laurance Tara  aliyeamua kujiunga na Chama hicho.(Hapa Mh Mbowe akimkabidhi Katiba ya Chadema Bw, Tara)

Karibu sana CHADEMA ushirikiane na Makamanda wenzio ila sisi huwa hatuvai tai kwahiyo baada ya hapa ukavae sare ya Chadema.

Hapa Mh, Mbowe akisain Kadi ya Bw, Tara
Hawa ni baadhi ya wajumbe wa kikao cha Baraza kuu la Chadema

Waandishi wa habari pia walikuwepo

No comments:

Post a Comment