Sunday, January 27, 2013

CHUO CHA KODI CHAWATUNUKU VYETI WAHITIMU 435 WAKIWEMO WAHITIMU NANE KUTOKA BOTSWANA KATIKA MAHAFALI YA TANO YA CHUO HICHO

Chuo cha Kodi Tanzania leo Kimefanya Mahafali yake ya Tano ya chuo hicho kilichopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Akisoma Risala yake katika Mahafali hayo, Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho Prof Palmagamba Kabudi  amesema kuwa kwa kipindi hichi cha  Mwaka 2011/2012 Chuo cha Kodi kimewatunuku wahitimu 435 ambapo miongoni mwao wahitimu 137 sawa na asilimia 31 ni wanawake.

Amesema kuwa, kuhitimu wanawake 137 ni hatua muhimu kwao katika jitihada zao za  kuwa na wahitimu wengi wanawake.

"Wanawake 137 ni wengi sana kwa hivyo sisi tunaona kuwa tumepiga hatua kubwa kwani jitihada zetu zote ni kuwa na wanawake wengi watakao hitimu katika Chuo chetu" amesema Prof Kabudi.
Miongoni mwa wahitimu waliotunukiwa vyeti, walikuwepo wafanyakazi nane kutoka Botswana Unified Revenue Service waliotunukiwa vyeti ambapo Prof Kabadi amemshukuru Kamishna Mkuu wa Botswana Unified Revenue Service Bw, Keneilwe Robert Morris kwa uamuzi wa kuwapeleka baadhi ya Maofisa wa Forodha na Kodi wa Botswana kwa ajili ya Mafunzo katika Chuo hicho.

Mahafali hayo yamehudhuriwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha Mh, Saada Mkuya Salum ambaye ndiye aliyekuwa Mgeni Rasmi katika Mahafali hayo, pamoja na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw, Harry Kitillya pamoja na Naibu wake Bw, Richard Bade.

Aidha Kamishna Mkuu wa Botswana Unified Revenue Service Bw, Keneilwe Robert Morris alikuwepo kwenye Mahafali hayo akishuhudia wahitimu nane kutoka Butswana waliokuwa wanapata Mafunzo katika Chuo hicho

No comments:

Post a Comment