Sunday, January 27, 2013

KABWE ZITTO ATOA YA MOYONI KUHUSU UVUNJIFU WA AMANI MKOANI MTWARA KUHUSU GESI

Mbunge wa Kigoma Kaskazini  Kabwe Zitto, akizungumza 
katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, 
kuhusu uvunjifu wa amani uliotokea mkoani Mtwara kutokana na nia ya Serikali kusafirisha gesi kwenda Dar es Salaam. 
(PICHA NA DOTTO MWAIBALE)



Na Dotto Mwaibale

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini Kabwe Zitto amelaani 
matukio ya uvunjifu wa amani, uharibu wa mali na mauaji yaliyotokea mkoani Mtwara yakihusishwa na nia ya serikali ya kusafirisha gesi kwenda Dar es Salaam.

Akizungumza katika mkuatnao na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, alisema hali iliyopo mkoani humo inasikitisha sana maana mali za wananchi zinaharibiwa, nyumba zinachomwa moto na watu wanapoteza maisha.

"Tunalaani matukio hayo kwa nguvu zetu zote maana 
kinachotokea Mtwara si Utanzania tusipowasikiliza wananchi hao na kutatua mgogoro huo kwa kuwashirikisha hali itazidi kuzorota wakati tukitupiana lawana" alisema Zitto.

Alisema katika kipindi cha wiki nne sasa kumekuwa na maandamano, malumbano na vurugu kuhusu mradi wa 
kujenga bomba la kusafirisha gesi asilia kutoka mkoani humo kwenda Dar es Salaam.

Alisema mradi huu wa kutandaza bomba la urefu wa kilometa 542 ni mkubwa sana hapa nchini na umathamani kubwa zaidi kul;iko miradi mingine yote ya miundombinu iliyopata kutokea hapa nchini.

" mradi huu utajengwa kwa mkopo wa dola za  Kimarekani 1.2 bilioni kutoka Benki ya Exim ya China" alisema Zitto.

Alisema tangu maandamano hayo yatokee Wizara yenye dhamana ya mradi huo imekuwa ikitoa matamko kwenye vyombo vya habari badala ya kwenda mkoani humo kuzungumza na wananchi, kusikiliza madai yao na kuona namna ya kutekeleza madai hayo.

Zito alisema wakati huu si wa kurumbana wala kumtafuta mchawi bali ni viongozi husika kwenda mkoani huo kutafuta suluhu ya jambo hilo na kuwaomba wananchi wa mkoa huo kutulia wakati suala lao linafanyiwa kazi badala ya kuzodoana na kurushia maneno wakati nchi ikiendelea kuungua.

Alisema yanayotokea Mtwara ni fundisho kwa Taifa namna ya kukabili changamoto za utajiri wa rasilimali, ili kuweka mkakati,  mambo haya yanayotokea mkoani humo yasitokee tena Tanzania.

Alisema maafa hayo yanaweza kuzuilika iwapo utakuwepo uwazi katika mikataba, kuwashirikisha wananchi kwenye rasilimali za nchi na kuwepo na uwajibikaji na si kufanya mambo hayo kwa siri jambo litakalotafsiriwa kama mradi husika upo kwa manufaa ya wachache.

No comments:

Post a Comment