Akizungumza katika Uzinduzi wa Mpango huo, Diwani wa Kata ya Kipawa Mhe, Bonnah Kaluwa, amesema kuwa Mpango huo utasaidia kuweka mazingira ya kata hiyo katika hali ya Usafi ambapo itaboresha afya za wakazi wa Kipawa.
Diwani Kaluwa amesema kuwa Mpango huo unadhaminiwa na watu wa Marekani lakini Dhamana itaanza baada ya jitihada ya wakazi wa Kipawa kuonekana.
Kwa upande wake Ofisa Utamaduni Msaidizi katika Ubalozi wa
Marekani, Bi, Shamsa Suleiman amesema kuwa wapo tayari kusaidia Kuboresha Mazingira Bora kwa Elimu katika kata hiyo.
Diwani wa Kata ya Kipawa Bonnah Kaluwa akitoa neno fupi katika hafla ya uzinduzi wa mradi huo |
Ofisa Utamaduni Msaidizi katika Ubalozi wa Marekani, Shamsa Suleiman, akitoa neno fupi katika uzinduzi huo. Marekani imeonesha nia ya kufadhili mradi huo. |
Mwenyekiti wa Kamati ya Shule ya Msingi Minazi Mirefu, Daniel Mwamasika, akiwasalimia wananchi na wageni waalikwa waliofika katika uzinduzi huo. |
No comments:
Post a Comment