Mechi
namba 92 ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyochezwa jana (Januari 27 mwaka huu)
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa Simba kuibuka na
ushindi wa mabao 3-1 limeingiza sh. 53,756,000.
Watazamaji 9,408 walikata
tiketi kushuhudia mechi hiyo iliyochezwa kwa viingilio vya sh. 5,000,
sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipatamgawo wa sh. 12,499,752.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 8,200,067.80.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni
asilimia 15 ya uwanja sh. 6,355,806.33, tiketi sh. 3,183,890, gharama za
mechi sh. 3,813,483.80, Kamati ya Ligi sh. 3,813,483.80, Mfuko wa
Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,906,741.90 na Chama cha Mpira wa
Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,483,021.48.
|
Sunday, January 27, 2013
PAMBANO LA LYON, SIMBA LAINGIZA MIL 53/-
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment