Shirika lisilo la Kiserikali la kutetea watu wenye Ulemavu
wa Ngozi Under The Same Sun (UTSS) limetoa Vyeti kwa walemavu wa Ngozi 43 waliohitimu ngazi mbalimbali za Elimu kwa
kusomeshwa katika vyuo mbalimbali na Shirika hilo.
Akizungumza katika Hafla ya Utoaji wa Vyeti hivyo
iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam nchini Tanzania, Mwenyekiti wa IPP Bw Reginald Mengi ambaye
ndiye aliyekuwa Mgeni Rasmi, amewapongeza wahitimu hao kwa kuhitimu na kuwataka
kujiamini na kuamini kuwa na wao wanaweza wakiwa mahali popote.
Bw, Mengi pia amewapongeza sana Shirika hilo kwa kuwasomesha
walemavu wa Ngozi kwani wamewapa ujasiri wa kujiamini kuwa wanaweza kufanya
lolote katika jamii na jamii ikawakubali.
“Unatakiwa ujikubali kuwa nawewe unaweza na unaweza ukawa
namba moja kati ya watu wengi, binafsi nawapongeza sana UTSS kwa kuwawezesha
walemavu wa Ngozi kupata Elimu bora “amesema Dk Mengi.
Katika Warsha hiyo iliyofanyika leo katika hoteli ya Serena
jijini Dar es Salaam Baadhi ya Makampuni ilijitolea kuajiri wahitimu 20 ambao
walikuwa tayari kupata Ajira kwani wengine waliopata vyeti bado wanaendelea na
masomo yao.
Peter Ash akikabidhi Cheti kwa Mmoja wa wahitimu katika Hafla
hiyo.
|
Mkurugenzi na Muhasisi wa UTSS Canada na Tanzania Bw Peter
Ash akiwapongeza wahitimu katika Hafla hiyo.
|
Wahitimu wakiwa kwenye Picha ya Pamoja na Mgeni Rasmi pamoja
na Uongozi wa UTSS.
|
Waajiri kutoka katika Makampuni mbalimbali waliojitolea kuwa ajiri wahitimu hao |
Wadau mbali mbali waliohudhuria katika Hafla hiyo.
|
Mwanamuziki mlemavu wa Ngozi akitoa Burudani katika Hafla hiyo |
No comments:
Post a Comment