Mkurugenzi katika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania,
Godwin Seiya (kushoto) akikabihdi mfano wa hundl wa shilingi milioni tano kwa
Mkurugenzi wa wa Huduma za Afya wa Hospitali ya Aga Khan Dr. Jaffer Dharsee
(kulia) ikiwa ni mchango wa benki hiyo wa kusaidia kampeni ya saratani ya
matiti inayolenga kujenga uelewa juu ya ugonjwa huo. (Na Mpiga Picha Wetu)
Mkurugenzi katika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania,
Godwin Seiya (kushoto) akikabihdi hundl
ya shilingi milioni tano kwa Mkurugenzi wa wa Huduma za Afya wa Hospitali ya
Aga Khan Dr. Jaffer Dharsee (kulia) ikiwa ni mchango wa benki hiyo wa kusaidia
kampeni ya saratani ya matiti inayolenga kujenga uelewa juu ya ugonjwa huo.
Mkurugenzi
katika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania, Godwin Seiya
(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kuchangia kampeni
ya saratani ya matiti inayoongozwa na hospitali ya matiti. Katikati ni
Mkurugenzi wa wa Huduma za Afya wa Hospitali ya Aga Khan Dr. Jaffer
Dharsee.
Na Mwandishi Wetu
BENKI
ya Azania imetoa shilingi milioni tano kwa Hospitali ya Agha Khan
zitakazosaidia kupiga jeki kampeni za kukuza uelewa wa saratani ya
matiti.
Akizungumza
katika hafla fupi ya makabidhiano ya fedha hizo mwishoni mwa wiki
jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Benki ya Azania katika ofisi ya
Mkurugenzi Mtendaji (Hazina na Maendeleo ya Biashara) Godwin Seiya,
alisema kuwa benki yake imejikita katika kusaidia masuala mbalimbali ya
kijamii ikiwa sehemu ya mchango wa benki hiyo kwa jamii.
Bw.
Seiya alisema kuwa benki yake imeamua kuunga mkono kampeni ya saratani
ya matiti ili kuwashawishi wanawake na jamii kwa ujumla kufanya
uchunguzi wa ugonjwa huo ili kupunguza hatari kwa wanawake wengi kupata
ugonjwa huo siku za usoni.
“Taarifa
zinaonyesha kuwa zaidi ya wanawake milioni moja na laki tano wanatatizo
la saratani ya matiti. Tanzania ina jumla ya wagonjwa 1,307 wa saratani
ya matiti. Sisi benki ya Azania tunaamini kuwa njia pekee ya kupunguza
tatizo hili ni kupitia kampeni.
“Tunaamini
kuwa kwa kutoa taarifa sahihi, waathirika wa saratani ya matiti
wanaweza kupata matibabu mapema na kuongeza nafasi yao kuendelea kuishi.
Leo
hii tunachangia shilingi milioni tano kuunga mkono kampeni ya mwaka huu
ambayo inalenga kukuza uelewa wa saratani ya matiti,” alisema.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi wa Huduma za Afya wa Hospitali ya Agha Khan,
Dkt. Jaffer Dharsee wakati wa hafla hiyo alisema kuwa kampeni ya mwaka
huu inalenga kufanyia uchunguzi zaidi ya wanawake elfu tano nchi nzima .
Dharsee
alisema kuwa kampeni za mwaka jana zilizofanyika katika mikoa ya Dar se
salaam, Mtwara, Dodoma na Lindi zilitumia zaidi ya dola za kimarekani
laki moja (Shilingi milioni mia moja na sitini) ambapo wanawake zaidi ya
elfu tatu walifikiwa na kampeni katika mikoa hiyo minne.
“Tutaendelea
na kampeni mwaka huu na lengo letu ni kuwafikia wanawake zaidi ya elfu
tano nchi nzima mwaka huu. Pia tutajumuisha na uchunguzi wa saratani
katika shingo ya kizazi mwaka huu. Tunaasa makampuni mengine ya biashara
kuunga mkono kampeni hizi,” alisema.
No comments:
Post a Comment