DAR ES SALAAM, Tanzania
MENEJIMENTI
ya NMB imewaonya wateja wake na umma kwa ujumla kuwa imegundua kwamba kuna
taasisi inayojitambulisha kama Tanzania Loans Society inadai kuwa mshirika wa benki
hiyo katika kutoa huduma za kibenki.
Taasisi
hiyo imedaiwa kuwa kwa kutumia mtandao wake wa intaneti imekuwa ikijinasibu kutoa
mikopo ambayo fedha zake zimeidhinishwa na NMB kupitia kwa mameneja wa matawi.
Aidha,
Tanzania Loan Society pia inadaiwa kueleza kwamba fomu za maombi ya mkopo na
malipo ya usajili vinaweza kulipwa kwa
kutumia namba ya simu ya mkononi.
Menejimenti
ya NMB imezidi kuwatahadharisha wateja wake na umma kwa ujumla kwamba haina ushirika
au makubaliano yoyote na taasisi hiyo katika shughuli zake.
Imeongeza
kuwa, NMB hutoa mikopo yake kupitia matawi yake tu, na hakuna namna yoyote ambayo inaweza kusababisha
gharama za maombi ya mikopo au mikopo
kutolewa kupitia simu za mkononi.
No comments:
Post a Comment