Wednesday, February 27, 2013

HII NDIYO TAARIFA KAMILI YA WALIOKUTWA WAKICHUKUA HELA KWENYE ATM YA NMB RUNGWE



Kamanda Diwani RPC Mbeya


WILAYA YA RUNGWE- JALADA LA UCHUNGUZI.
MNAMO TAREHE 25.02.2013 MAJIRA YA SAA 20:40HRS HUKO KATIKA BENKI YA NMB TAWI LA TUKUYU LILILOPO TUKUYU MJINI WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA. POLISI WILAYA YA RUNGWE WALIWAKAMATA. 1. JUMANNE S/O MAGERE, MIAKA 29, MFANYABIASHARA YA DUKA MKAZI WA MLOWO – MBOZI 2. JUMA S/O KABYELO, MIAKA 20, MJALUO, MFANYABIASHARA YA DUKA, MKAZI WA MSASANI- TUKUYU 3. JOSEPH S/O PETTER, MIAKA 20, MKURYA, MKULIMA, MKAZI WA MSASANI- TUKUYU NA 4. MIRAJI S/O KETAHA,MIAKA 34,MFANYABIASHARA YA DUKA  MKAZI WA MSASANI-TUKUYU WAKIWA NA KADI 150 ZA ATM ZA WATU MBALIMBALI WAKIWEMO WATUMISHI WA SERIKALI  AMBAPO TAYARI WALIKUWA WAMESHATOA KIASI CHA TSHS 20,543,000/= KUTOKA KATIKA MASHINE YA ATM . BAADA YA KUHOJIWA  MTUHUMIWA JUMANNE S/O MAGERE ANAKIRI KUWASHIRIKISHA WATUHUMIWA WENZAKE KUMSAIDIA KUTOA KIASI HICHO CHA PESA NA KWAMBA KADI HIZO NI MALI YA WATEJA WAKE  AMBAO WENGI NI WILAYA YA MBOZI WALIOKOPA VITU MBALIMBALI KATIKA DUKA LAKE ANALOUZA BIDHAA ZINAZOTUMIA UMEME ZIKIWEMO REDIO,TELEVISION PIA VYEREHANI,MAGODORO NA BAISKELI NA KUWA WATEJA WAKE NDIO WALIOMPATIA KADI HIZO PAMOJA NA NAMBA ZAO ZA SIRI [PASSWORD] ILI AWEZE KUKATA DENI ANALOWADAI NA KUWAPATIA KIASI CHA PESA KINACHOSALIA. KUFUATIA TUKIO HILO WATUHUMIWA  WAMEENDELEA KUHOJIWA KITUO CHA POLISI TUKUYU-RUNGWE WAKATI PIA UFUATILIAJI UKIFANYWA KWA  WENYE KADI HIZO ZA ATM. UFUATILIAJI UNAFANYWA PIA  KUONA KAMA KUNA UKOPESHAJI WA FEDHA TASLIMU UNAOHITAJI MALIPO NA RIBA ILI HATUA ZINAZOSTAHILI KISHERIA ZIWEZE KUFUATWA. HADI SASA UCHUNGUZI HAUJABAINI WIZI WA MOJA KWA MOJA ULIOFANYWA NA WATUHUMIWA KAMA ILIVYORIPOTIWA NA BAADHI YA VYOMBO VYA HABARI WALA HAKUNA TAARIFA YA MTU KUIBIWA KWENYE AKAUNTI YAKE. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI  DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO  KWA  WANANCHI KUWA MAKINI SANA NA “TRANSACTIONS” ZINAZOHUSU AKAUNTI ZAO KWA KUWA KUMEKUWA NA MALALAMIKO KADHAA YANAYOFIKISHWA VITUO VYA POLISI LAKINI YAKIFUATILIWA INABAINIKA KUWA CHANZO NI UTOAJI HOLELA WA NAMBA YA SIRI YA MWENYE AKAUNTI.

                                                                           
Signed By,
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
   KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments:

Post a Comment