Mwl. Salome Makanza wa Shule ya msingi Oysterbay akisoma risala kwa
niaba ya Mwl. Mkuu Msaidizi Janeth Mdingi ambapo ameishukuru Hoteli ya
DoubleTree by Hilton kwa kubuni kampeni kama hiyo ya kugawa taa
zinazotumia Nishati ya Jua kwa Wanafunzi wa Darasa la Saba ambao
wanakabiliwa na Mitihani kwani zitawasaidia hata Umeme utakapokatika
majumbani mwao.
Mwl. Salome Makanza akikabidhi risala yake kwa Mgeni rasmi Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais
Mh.Dkt. Terezya Huvisa. Kulia ni Mkurugenzi wa kanda wa Hoteli ya
DoubleTree by Hilton Dar es Salaam Bw. Judd Lehmann. Kuhsoto ni Kushoto
ni Afisa Elimu Msaidizi wa Wilaya ya Kinondoni Faustin Kikove na
Mwl.Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Oysterbay Bi. Janeth Mdingi (wa
pili kushoto).
Meza Kuu katika Halfa ya Uzinduzi wa taa zinazotumia Nishati ya Jua
zilizotolewa na Hoteli ya DoubleTree by Hilton ya Jijini Dar es Salaam
kwa shule za msingi za Mikoa ya Dar es Salaam ambapo leo wamezindua
kampeni hiyo kwa kuanzia shule ya Msingi Oysterbay jijini.
Mkurugenzi wa Kanda wa Hoteli ya DoubleTree by Hilton ya Dar es Salaam
Bw. Judd Lehmann akizungumza wakati wa kuzindua kampeni ya kugawa taa
zinazotumia Nishati ya Jua kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi za Mkoa wa
Dar es Salaam ambapo amesema lengo lao ni kutaka wanafunzi hao wawe na
ufahamu kuhusiana na Nishati mbadala ya Umeme ambayo ni rafiki wa
Mazingira.
Hivyo taa hizo zitawasaidia hata kunapokuwa hakuna Umeme wa Tanesco kujisomea majumbani bila kipangamizi.
Na Mwandishi wa MoBlog
Hoteli ya DoubleTree by Hilton jijini Dar es Salaam imezindua rasmi kampeni ya matumizi ya nishati ya jua ambayo itadumu kwa muda wa miaka miwili katika shule za mkoa wa Dar es Salaam.
Katika kampeni hiyo Hoteli ya DoubleTree by Hilton itakuwa ikigawa taa 200 za mezani zenye kutumia nishati ya jua kwa wanafunzi wa darasa la saba kwa shule tofauti kila mwezi, lengo likiwa nikuwafanya wawe na ufahamu zaidi juu ya chanzo kingine cha umeme ambacho ni rafiki wa mazingira kwa kupitia mafunzo katika madarasa yao.
Akizindua rasmi kampeni hiyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh. Dkt. Terezya Huvisa ameupongeza uongozi wa hoteli hiyo kwa kubuni kampeni ambayo itawasaidia wanafunzi kutambua umuhimu wa nishati ya jua na kufaidika na taa wao na familia zao.
Mh. Huvisa amegawa awamu ya kwanza ya taa 200 za mezani zinazotumia nishati ya jua kwa wanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya msingi Oysterbay na kuwataka wazitunze na kuzitumia kujisomea.
Naye Mkuu wa hiyo amtoa shukrani kwa Hoteli ya DoubleTree by Hilton akisema kampeni hiyo inazo faida nyingi kwa upande wa afya, elimu, uchumi wa nyumbani na mazingira kwa ujumla.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Ofisi ya Makamu wa
Rais Mh. Dkt. Terezya Huvisa akitoa hotuba kuzindua kampeni ya ugawaji
taa zinazotumia Nishati ya Jua iliyobuniwa na Hoteli ya DoubleTree By
Hilton jijini Dar kwa wanafunzi wa shule za msingi ambapo ameipongeza
hoteli hiyo kwa kubuni mradi kama huo kwani taa hizo kwa kuwa zinatumia
Nishati ya jua zitawasaidia wanafunzi kujisomea na familia zao pia
kupata Mwanga kunapokuwa tatizo la kukatika kwa Umeme.
Aidha amewaasa wanafunzi hao kuzitunza taa hizo na kuzitumia kwa maelngo yaliyokusudiwa.
Baadhi ya Wanfunzi wa Darasa la Saba wa Shule ya Msingi Oysterbay wakimsikiliza mgeni rasmi.
Baadhi ya wageni waalikwa na wafanyakazi wa hoteli ya DoubleTree by Hilton ya jijini Dar wakati wa uzinduzi huo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Ofisi ya Makamu wa
Rais Mh. Dk. Terezya Huvisa akiendesha maswali ya masuala ya mazingira
kupima upeo wa uelewa kwa Wanafunzi wa shule ya msingi Oysterbay jijini
Dar es Salaa wakati akizindua kampeni ya kugawa taa zenye kutumia
Nishati ya jua kwa shule za msingi za mkoa wa Dar iliyodhaminiwa na
Hotel ya Doubletree by Hilton ya jijini Dar.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Ofisi ya Makamu wa
Rais Mh.Dkt. Terezya Huvisa akimtunza Mwanafunzi Neema Njau shilingi
Elfu taslim baada ya kujibu vyema maswali yanahusiana na Mazingira
wakati wa hafla ya uzinduzi wa taa zinazotumia Nishati ya Jua
zilizogaiwa kwa wanafunzi wa Darasa la saba wa shule ya msingi Oysterbay
jijini Dar.
Mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Ofisi
ya Makamu wa Rais Mh. Dkt. Terezya Huvisa akikata utepe kuashiria
uzinduzi rasmi wa taa zinazotumia Nishati ya Jua zilizotolewa na Hotel
ya Doubletree by Hitlon kwa ajili ya kugawa kwa wanafunzi wa shule
tofauti za msingi mkoa wa Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo
Mkurugenzi wa Kanda wa Hoteli ya DoubleTree by Hilton ya Dar es Salaam
Bw. Judd Lehmann aliyeambatana na Meneja Mkuu wa Hoteli hiyo Bw. Sven
Lippinghof (mwenye tai ya Orange) na Mkurugenzi wa Masoko Hoteli ya
DoulbeTree by Hilton Florenso Kirambata (nyuma ya Waziri). Kushoto
(mwenye kipaza sauti ) ni Afisa Elimu Msaidizi wa Wilaya ya Kinondoni
Faustin Kikove na Mwl. Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Oysterbay Bi.
Janeth Mdingi (wa tatu kushoto).
Mgeni rasmi Mh. Dkt. Terezya Huvisa akihamasisha wanafunzi kutumia
vizuri taa hizo hasa nyakati za kujisomea ya kukabidhi rasmi. Mkurugenzi
wa kanda wa Hoteli ya DoubleTree by Hilton Dar es Salaam Bw. Judd
Lehmann (wa tatu kulia), Meneja Mkuu wa Hoteli hiyo Bw. Sven Lippinghof
(wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Masoko Hoteli ya DoulbeTree by Hilton
Florenso Kirambata (kulia) na Wa kwanza Kushoto ni Afisa Elimu Msaidizi
wa Wilaya ya Kinondoni Faustin Kikove na Mwl Mkuu Msaidizi wa Shule ya
Msingi Oysterbay Bi. Janeth Mdingi (wa pili kushoto).
Mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Ofisi
ya Makamu wa Rais Mh. Dkt. Terezya Huvisa akikabidhi rasmi taa
inayotumia Nishati ya jua kwa mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo John
Maganga. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkurugenzi wa kanda wa Hoteli ya
DoubleTree by Hilton Dar es Salaam Bw. Judd Lehmann (kulia) na Kushoto
ni Afisa Elimu Msaidizi wa Wilaya ya Kinondoni Faustin Kikove na Mwl
Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Oysterbay Bi. Janeth Mdingi (wa pili
kushoto).
Mkurugenzi wa kanda wa Hoteli ya DoubleTree by Hilton Dar es Salaam Bw.
Judd Lehmann akikabidhi moja ya taa hizo kwa mwanafunzi wa darasa la
saba Rebecca Andrew.
Mkurugenzi wa Masoko Hoteli ya DoubleTree by Hilton Florenso Kirambata
akifanya vivyo hivyo kwa mmoja wa wanafunzi wa shule msingi Oysterbay.
Mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Ofisi
ya Makamu wa Rais Mh. Dkt. Terezya Huvisa akiwa kwenye picha ya pamoja
na Uongozi wa Hoteli ya DoubleTree By Hilton, Uongozi pamoja na baadhi
ya wanafunzi wa shule ya msingi Oysterbay baada ya kukabidhi taa hizo.
MC wa shughuli hiyo Taji Liundi akifurahi jambo na Meza kuu.
Mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Ofisi
ya Makamu wa Rais Mh. Dkt. Terezya Huvisa akiteta jambo na Mkurugenzi wa
kanda wa Hoteli ya DoubleTree by Hilton Dar es Salaam Bw. Judd Lehmann
wakati wa hafla hiyo. Kushoto ni Mwl. Mkuu Msaidizi wa Shule hiyo Janeth
Mdingi.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Oysterbay ya Jijini Dar es Salaam wakipozi
na taa zinazotumia Nishati ya jua ambazo zimetolewa na Hoteli ya
DoubleTree by Hilton. Wanafunzi hao wameishukuru Hoteli hiyo na kusema
taa hizo zitawasaidia kujisomea hata kipindi ambacho Umeme umekatika
majumbani hivyo kuongeza uwezo wao kielimu.
No comments:
Post a Comment