Monday, February 11, 2013

TTCL YAUNGANISHA OFISI ZA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI NA MKONGO WA TAIFA WA MAWASILIANO



 MAKABIDHIANO: Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali Bw. Ludovick Utoh (kushoto) akipokea mkataba wa kumalizika kwa mradi  wa awamu ya kwanza wa vituo 11 kutoka kwa Mkuu wa Mauzo kutoka Kampuni ya SimuTanzania (TTCL), Bw. Tambwe Kisamba.
 Baadhi ya wafanyakazi wa TTCL  na NAO wakimsikiliza Bw. Utoh
 Wafanyakazi wa Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi kutoka Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL).

 DAR ES SALAAM,Tanzania

Kampuni ya simu Tanzania (TTCL) imekabidhi vituo 11 vilivyounganishwa na mkongo wa taifa kwa mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali uliogharimu shilingi milioni 477.

Akiongea katika halfa hiyo mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali Bw. Ludovick Utoh ameishukuru TTCL kwa kukamilisha awamu ya kwanza ya mradi huo, na kuongeza kuwa uwepo wa mawasiliano hayo kutasaidia ofisi zote za mkaguzi wa hesabu za serikali kuwa salama zaidi na kutaongeza uadilifu kwani watakuwa na uwezo wa kuzuia tovuti ambazo hazina manufaa katika utendaji wa kazi.

Aliongeza kuwa, faida nyingine ya mawasiliano hayo kutawawezesha kuanzisha mawasiliano ya ndani "intranet" hivi karibuni baada ya kupata mtandao wa uhakika kutoka TTCL, pia  kupunguza kazi za makaratasi kwani sasa watakuwa wanatumia zaidi barua pepe kuwasiliana badala ya kuandikiana ujumbe mfupi kwa njia ya karatasi, kuwa na uwezo kwa kupokea taarifa kutoka mikoa mbalimbali kwa njia ya mtandao badala ya mtu kusafiri kutoka mkoani kuleta ripoti Makao Makuu.

Naye Mkuu wa Mauzo kutoka Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Kisamba Tambwe amemuahidi Mkaguzi na Mdhibiti mkuu wa hesabu  za serikali kuwa, TTCL itakuwa bega kwa bega kuhakikisha inawasaidia pale watakapohitaji msaada kutoka TTCL na itawapa mafunzo watu wa ufundi kutoka Ofisi za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ili waweze kutatu a matatizo madogo madogo ya kiufundi endapo yatatokea.

No comments:

Post a Comment