MKUU wa Wiliya ya Temeke, Dar es Salaam, Bi. Sophia Mjema,
amewaagiza Wenyeviti wa Serikali za Mitaa na Maofisa Watendaji wote wilayani
humo, kuwachapa viboko wanawake na wanaume wanaovaa nusu uchi ili kulinda
maadili ya Kitanzania.
Bi. Mjema alitoa agizo hilo Dar es Salaam jana alipofanya ziara katika Kata ya Keko, Tarafa ya Chang'ombe wilayani humo ili kusikiliza kero na wananchi na changamoto walizonazo watendaji.
Ziara hiyo ni moja ya mikakati aliyojiwekea ya kutembelea kata zote wilayani humo. Bi. Mjema aliwataka viongozi wa kata hiyo, kutofumbai macho kuhakikisha wananchi wanaowaongoza,
wanajiheshimu kwa kuvaa mavazi ya heshima.

Mnapowakuta wanawake na wanaume wanaovaa nusu uchi,
muwachukulia hatua kwa kuwapa adhabu ya viboko pamoja na kuwafikisha mahakamani
ili iwe fundisho kwa wengine.
Msiwe na hofu ya kuchukua uamuzi huo sheria zinazowalinda zipo na mkikwama, mripoti maara moja katika ofisi yangu...nyie ni viongozi wa Serikali katika kata hivyo lazima tuwe na Taifa linalozingatia maadili.

Aliongeza kuwa, kama hali hiyo isipodhibitiwa mapema Taifa
litakuwa na vijana legelege, makahaba, majangili, makaka poa pamoja na ongezeko
la machangudoa jambo ambalo ni hatari.
Katika hatua nyingine, Bi. Mjema aliwaagiza viongozi hao kuhakikisha wanafunzi wanaokaa katika magenge ya wahuni
na kumbi za starehe badala ya kwenda shule, wanakamatwa, kuchapwa viboko na kupelekwa shule kwa lazima.

Mkiwakamata kwanza wachapeni viboko, kuwapa elimu ili
watambue umuhimu wa kusoma na kuwapeleka katika shule zao, hatuwezi kuruhusu
wazurure hovyo mitaani na kucheza
kamali huku ni kuzalisha bomu kubwa kwa Taifa.
kamali huku ni kuzalisha bomu kubwa kwa Taifa.
Aliwataka Maofisa Watendaji wote kutotoa vibari kwa vikundi
mbalimbali vinavyopiga muziki masaa 24 na kusababisha wananchi kutopata muda
mzuri wa kupumzisha akiri zao baada ya kazi.
Katika baadhi ya maeneo yanayopiga muziki masaa 24, jirani
zao ni wagonujwa lakini wahusika wamepewa vibali...kuanzia leo vibari vyote vya
aina hii vipitie kwangu ili kuona kama kuna ulazima wa kufanya hivyo.
Alisema baa zote zinazofunguliwa kuanzia saa nne
asubuhi ni marufuku kwani muda huo ni wa kazi kwa kila mwananchi ambaye
anapaswa kujitafutia siziki si vinginevyo.Aliongeza kuwa, wamiliki wa baa ambao watakiuka agizo hilo watachukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani ambapo watendaji wote, wasitoe vibari vya kuruhusu hali hiyo.
---
via gazeti la Majira
No comments:
Post a Comment