Sunday, March 3, 2013

ERNANDEZ NJE SIKU 15 BARCELONA, KUIKOSA AC MILAN



BARCELONA, Hispania

Nyota huyo ambaye alirejea kutoka tatizo la majeraha na kumudu kucheza mechi dhidi ya AC Milan ya Italia na Sevilla, na sasa yu shakani kuwahi pambano la marejeano mtoano wa 16 bora Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Milan hapo Machi 12
KIUNGO wa FC Barcelona, Xavi Hernandez jana alilazimika kulikosa pambano la mahasimu ‘El Clasico’ dhidi ya Real Madrid lililoisha kwa kikosi cha kulala mabao 2-1 na anatarajia kuwa nje ya uwanja kwa siku 15 kutokana na kuumia nyama za paja, Barca ilisema juzi katika taaifa yake.

Xavi nyota wa kimataifa wa Hispania, alirejea tatizo lake la misuli katika pambano lililoisha kwa kikosi chake kulala nyumbani Nou Camp kwa mabao 3-1 na kutolewa katika Kombe la Mflame na Madrid – mechi iliyopigwa Jumanne iliyopita.

Nyota huyo ambaye alirejea kutoka tatizo la majeraha na kumudu kucheza mechi dhidi ya AC Milan ya Italia na Sevilla, na sasa yu shakani kuwahi pambano la marejeano mtoano wa 16 bora Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Milan hapo Machi 12.

"Mechi dhidi ya Milan na Madrid, hatukuwa wazuri kama ilivyo kawaida yetu, lakini sio sababu ya kutufanya tukate tama dhidi yao," alisema Kocha Msaidizi wa Barca, Jordi Roura kuviambia vyombo vya habari kuelekea mechi ya jana usiku na ile ya Machi 12.

"Timu inatarajia kupiga hatua na kuwa tayari kushindana kwa kila kitu. Mtazamao chanya na upiganaji wa aina yake miongoni mwa wachezaji wetu – unastahili kupongezwa."

Roura, msaidizi wa Tito Vilanova, alikiri kikosi chake kuumia baada ya kuwaudhi mashabiki wa nyumbani kutokana na kichapo cha katikati ya wiki, lakini akasema njia bora ya kurejesha amani kwa wafuasi wao ni ‘kushindana na kupata matokeo mazuri.’

SuperSport.com

No comments:

Post a Comment