Monday, March 4, 2013

POLISI ARUSHA WATEKETEZA MASHAMBA YA BANGI


Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna 
Msaidizi
wa Polisi (ACP), Liberatus Sabas akishirikiana 

na askari wa jeshi hilo
(hawapo pichani), kuharibu mimea ya madawa ya 

kulevya aina ya bangi kwa kuikata na kisha 

kuichoma moto katika operesheni iliyofanyika 

wilayani Arumeru . (Picha habari na Janeth Mushi)
Kamanda Liberatus Sabas, akibeba begani mimea 
aina ya bangi tayari kwa kuikusanya kwapamoja 

na kisha kuichoma moto katika operesheni hiyo.
Hapa akifyeka shamba la bangi
Bangi iliyowekwa kwenye viroba ikiingizwa katika 
gari la polisi
Askari polisi wakiwa kwenye mashamba ilipolimwa 
bangi hiyo

RPC AONGOZA OPERESHENI HIYO

Na Janeth Mushi,Arusha

JESHI la Polisi mkoa wa Arusha kwa kushirikiana na vyombo vingine vya
usalama,vimefanikiwa kuteketeza Bangi iliyokuw aimeoteshwa katika
mashamba yanayokadiriwa kuwa na ukubwa wa hekari 150.

Aidha bangi hiyo ilikutwa katika vijiji vya Likamba na Imbibya
vilivyopo Wilayani Arumeru mkoani hapa,katika Operesheni iliyoongozwa
na  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP)
Liberatus Sabas,iliyoanza  majira ya asubuhi,Machi Mosi mwaka huu.

Mara baada ya kikosi hicho kufika katika kijiji cha Likamba
walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa watatu wlaiokuwa na viroba vyenye
bangi,pamoja na kufyeka na kuteteketeza kwa moto bangi iliyokuwa bado
haijavunwa.

Katika vijiji hivyo viroba vingi vya madawa hayo ya kulevya
vilionekana vikiwa vimefichwa katika mashamba ambaye yameoteshwa
mahindi,ambapo wenyeji wa maeneo hayo waliyahama makazi yao kw amuda
na kukimbilia maeneo ya milimani ya jirani.

Akizungumzia  tukio hilo  Kamanda Sabas alisema jumla ya viroba
vilivyopatikana ni 32 vyenye uzito tofauti huku watuhumiwa watatu
ambao ni JaluoTendevesi (32) na Tikayo Kilamee (23) wote wawili ni
wakulima na ni wakazi wa kijiji cha Ndevesi wilayani Arumeru pamoja na
Ngwerenya Siraitei (55) Mkulima Mkazi wa Mombo mkoa wa Tanga
walikamatwa.

ACP Sabas  alitumia fursa  hiyo kuwaomba Wataalamu wa kilimo
kuwatembelea wakazi wa maeneo hayo kwa lengo la kuwapa elimu ya kilimo
mbadala ili ardhi hiyo waitumie kwa kulima mazao  ya chakula na
biashara badala ya kuendelea na kilimo cha madawa hayo yenye madhara
makubwa kwa binadamu.

Alisema kuwa mafanikio hayo ni muendelezo wa ushirikiano mzuri baina
ya jeshi hilo na vyombo vingine vya usalama pamoja na wananchi ambao
kwa kiasi kikubwa wanatoa taarifa zinazohusu uhalifu na wahalifu kwa
jeshi hilo mara kwa mara.

Tangu kuanza kwa mwaka huu kwa kipindi cha mwezi
Januari-Februari,Jeshi hilo  limefanikiwa kukamata madawa ya kulevya
aina ya Mirungi viroba 372 vikiwa vinasafirishwa toka nchi jirani ya
Kenya kuingia nchini na pia madawa ya kulevya aina ya bangi  magunia
yapatayo 143 huku kesi za matukio hayo zikiwa zimeshafikishwa katika
vyombo vya sheria.

No comments:

Post a Comment