Wednesday, March 20, 2013

STORI KAMILI KUHUSU MKUCHIKA NA WENGINE KUINGIA KWENYE BARAZA LA WADHAMINI YANGA


.
.
Uongozi wa Yanga umetangaza baraza la Wadhamini wa klabu hiyo akiwemo mke wa aliyekua Rais wa Zanzibar hayati Abeid Karume, Francis Kifukwe pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala bora) George Mkuchika.
Akilitambulisha hilo baraza linalotarajiwa kuwa na watu saba, mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manji amesema “wao ndio wamepewa jukumu kwa  heshima ya kulinda mali za Yanga ambazo ni za Wanachama, hii NI mikataba muhimu ambayo tunatarajia kuingia, lazima tuwe na chombo huru ambacho kitakua kinatazama mali za Yanga kama zinalindwa au zinaendelezwa kama katiba inavyosema”
Kwenye sentensi nyingine, Manji amesema “mimi na kamati yangu tunatoka jasho, hii sio hadhi ya Yanga kushinda moja bila… ubingwa Mungu akipenda mwaka huu tutafanikiwa lakini sio moja bila, tushinde tatu bila, nne bila, tano bila.. kamati yangu ya utendaji kidogo tumegawanyika nguvu, tunakwenda kulinda mali na kwenda kushindana kwenye mpira… sasa naomba hili baraza la Wadhamini lipokewe vizuri”

No comments:

Post a Comment