Na Bryceson Mathias, Lukunguni Mvomero.
TUHUMA za
Ufisadi na uchakachuaji wa mifuko ya mbolea 600 ya mwaka 2012 na 2013 ya
Kijiji cha Lukunguni, Kata ya Kikeo, Mvomero Morogoro, zimewakasirisha
wanachama na viongozi wa Chama cha Mapinzuzi (CCM), ambapo wamekusanya
Kadi kwa Mwenyekiti wao na kutishia kutimkia Chadema.
Hayo yalisemwa
Jana na Mwenyekiti Serikali ya Kijiji hicho, Login Mnari, baada ya
Mkutano uliohusisha wajumbe 25 wa Serikali ya Kijiji, uliowahoji wenzao
11 waliorubuniwa na Viigogo wa Kata na Wilaya na kufanya Kikao cha Siri
kijiji Jirani ili waridhie hadaa kuwa walipokea Mbolea ya 2012/13 wakati
si Kweli !.
Mnari alidai
wajumbe walioamsha tishio la kutimkia Chadema baada ya kubanwa kwenye
kikao na kusaini muhutasi kukiri walirubuniwa na vigogo wa Kata na
Wilaya (na Gazeti kuona sahihi) ni, Mwenyekiti Umoja wa Wanawake wao
Viliginia Emili na Katibu CCM Tawi la Lukunguni Octaviani Kupeni.
“Vijana 43 wa
(UVCCM) kijijini wamenitupia Kadi, ambapo Mamia wakiwemo wa vijiji vya
jirani ambao wamechezewa mchezo mchafu kiasi cha kutumia hata majina ya
watu waliokufa kuwa walipokea Vocha za Mbolea (Ninazo); wamekasirishwa
na tukio hilo, na sasa wanadai wanatimkia Chadema”. alisema Mnari
Alipoulizwa
yeye na Wajumbe 24 wa Serikali ya Kijiji kama wanakiri hawakupokea Vocha
za Mbolea 450 za 2012 na Vocha 150 za 2013, wakazi wakitimkia Chadema
wao watachukua hatua gani? Alisema, “Kama wataendele kumung’unya maneno,
watakaobaki wabaki, lakini tulio wengi tutatimka kuepuka aibu”.
Alisema,
Mbolea hiyo ni Mifuko 150-Urea, 150-DAP, 150 ya Mahindi jumla 450 ya
2012. Nyingine ni Mifuko 50-Urea, 50-Minjingu, 50 (ya Mahindi) jumla
150.
Aidha Mapema
Diwani wa Kata ya Kikeo Exavery Msambara alipohojiwa na Mwandishi kuhusu
tuhuma ya Mbolea Mifuko 450 (2012) mwaka jana, alikanusha vikali
kuhusika na Ubadhirifu huo, ambapo alimtaka mwandishi wazunguke naye
kwenye ziara ya vijiji vya Kata, asikie kama anasutwa kuhusu mbolea,
jambo ambalo mwandishi aligoma.
No comments:
Post a Comment