Wednesday, April 17, 2013

VETA YATANGAZA USAJILI MPYA WA VYUO VYAKE: ILI VYUO VISAJILIWE UPYA LAZIMA VIUWE NA VIGEZO STAHILI


Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Eng, Zebadia Moshi akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu Matokeo ya Usajili Mpya wa Vyuo vya Ufundi Stadi.
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA),  imetangaza usajili Mpya wa Vyuo vya Ufundi stadi  kutokana na Mabadiliko ya Sayansi, Tecknolojia, kiuchumi na Mtangamano ulioko katika nchi za Afrika Mashariki na SADC.

Akizungumza na waandishi wa habari leo katika makao makuu ya VETA Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo Eng Zebadia Moshi amesema kuwa, Mabadiliko hayo yamesababisha, Mamlaka kufanya Mapitio tena ya Vigezo vinavyotumika katika kusajili vyuo vya vya Ufundi Stadi ili viweze kuandaa wanafunzi Mahiri watakao weza kuhimili Ushindani unaoletwa na Mabadiliko tajwa.

Eng Moshi, Ametaja Sifa Mpya za Kusajilili Chuo ni kama Ifuatavyo:
  1. Uongozi Bora vwa Chuo
  2. Vifaa vya Kufundishia Vya kutosha kulingana na Mitaala
  3. Majengo ya Kufundishia ya Kutosha na yenye Viwango vinavyotakiwa
  4. Uwezo wa kifedha wa chuo ikiwa ni pamoja na Utunzaji.
Ameendelea kusema kuwa Mpaka sasa Vyuo vilivyoomba Usajili ni Vyuo 732,na vilivyofikia vigezo vya kukaguliwa baada ya Kuchunguza maombi yao na kukaguliwa ni 480 katika mikoa tofautitofauti.

Aidha Eng Moshi amevitaka vyuo kuweka cheti cha Usajili wake katika Notice board ya Chuo na kuandika namba ya Usajili kwenye bango linaloonyesha chuo kilipo.

"Kwakuweka namba ya Usajili kwenye Notice board tutatambua vyuo visivyo vya VETA kwa namba ya Usajili," amesema Moshi.

No comments:

Post a Comment