Wednesday, May 1, 2013

BALOTELI AKIPAKA TENA!!





imageimageimage imageMoja ya vitu ambavyo siku zote ni vya uhakika ni vituko toka kwa staa wa soka wa nchini Italia Mario Balotelli ambaye kwa sasa anakipiga na klabu ya Ac Milan . Huuu jamaa vituko vyake viko kwenye chati na siku zote hajaacha kuwa ‘source’ ya headlines za habari eidha kwa kitu anachokifanya au kauli inayotoka mdomoni mwake .
Safari hii Balotelli ametoa kali ambayo hakuna ambaye aliwahi kutarajia toka kwake , Balotelli kama unavyoweza kutarajia toka mchezaji wa kiwango cha juu kama yeye anafuatilia michuano ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE hata kama timu yake ya Ac Milan haiko kwenye michuano hii na amekuwa akiufuatilia mchezo wa nusu fainali kati ya Real Madrid na Borrusia Dortmund ambao usiku wa leo utakuwa unapigwa kwa marudiano baada ya ule wa wiki iliyopita .
Madrid ilifungwa mabao manne na kama ilivyo kwa asilimia kubwa ya mashabiki Balotelli haamini kama Real Madrid inaweza kufanya maajabu ya kugeuza kipigo cha 4-1 na kufuzu kucheza fainali . Kudhihirisha hilo Balotelli ameweka nadhiri ya kuwaruhusu wachezaji wote wa Real Madrid kufanya ngono na mpenzi wake ambaye ni model wa Ubelgiji Fanny Neguesha endapo wataitoa Dortmund na kufuzu kucheza fainali .
Amini usiamini Balotelli ametoa kauli hiyo abayo imenukuliwana magazeti mawili makubwa ya Hispania Marca na As Ambapo amesema haamini kama Madrid wanaweza kurudi na kufanya maajabu.
Hadi sasa hakuna kauli yoyote toka kwa nyota wa Madrid kama Ronaldo , Ozil na Benzema pamoja na wenzao abaye amezungumzia ‘ofa’ hii ya kulala na mpenzi wa Balotelli endapo watashinda mchezo wa leo.

No comments:

Post a Comment