Saturday, May 18, 2013

WAKAZI ZAIDI YA 500 HAWANA PA KUISHI BAADA YA KUBOMOLEWA NYUMBA ZAO

Mwanamama aliyenaswa na Kamera yetu Maeneo ya Kivule jijini Dar es Salaam akiwa analia baada ya Polisi kubomoa makazi yake katika Maeneo hayo jambo lililopelekea Mpaka sasahivi Mwanadada huyu kukosa pa kuishi.
 Katika Kuitunza Amani ya Tanzania  inayoaminika kuwa imejaa Tele, Bado kuna wananchi wengine ambao ni Watanzania Wenzitu hawaifaidi na wanaona kama Amani haipo Kabisa kutoka na na Hali wanayoishi nao.

Hayo yametokea hivi karibuni, katika Kata ya Kivule jijini Dar es Salaam Baada ya Polisi kuvunja nyumba za Wakazi zaidi ya Miatano na kuharibu mali zao, ambapo, mpaka hivi sasa Wakazi hao hawana Pakuishi.

Chanzo cha Polisi kuwabomolea Makazi yao ni Mgogoro uliopo katika Eneo hilo ambao tayari kesi ipo mahakamani lakini polisi wameingilia uhuru wa Mahakama na kuvunja kesi ikiwa bado ipo Mahakamani.

Maasinda imeshuhudia baadhi ya picha za Eneo hilo, na kuona watu wakiishi kwa tabu kutokana na kukosa Makazi baada ya kubomolewa.
Hii ni Moja ya Nyumba iliyojengwa kwa Muda ili kuwasitiri wananchi waliobomolewa nyumba zao, mahali ilipo nyumba hiyo ya Muda kulikuwa na nyumba kubwa na nzuri iliyobomolewa na Askari hao.

Jionee Mwenyewe

Watu wazima waliotafuta hela kwa jasho jingi wakafanikiwa wakimwaga Machozi hadharani baada ya kubomolewa nyumba zao.

Yalitumika Mabomu kubomolewa Nyumba hizo hili ni Moja ya Kasha la Bomu

MAASINDA inatarajia kufika eneola Tukio na itawaletea hali ilivyo katika Maeneo hayo

No comments:

Post a Comment