Thursday, May 9, 2013

ZALISHENI KWA KUJALI MAZINGIRA NA AFYA ZA BINADAMU NI TANGAZO WAKATI WA SEMINA YA TBS NA SHIRIKA LA VIWANGO LA KIMATAIFA

Mashirika na Makampuni Mbalimbali nchini Tanzania wametakiwa kuzalisha Bidhaa zao kwa kujali mazingira na kujali afya za Binadamu wengine.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Masoko katika Wizara ya Viwanda na Bihashara Bw, Odilo Majengo, katika Warsha iliyoandaliwa na TBS pamoja na Shirika la Viwango la Kimataifa  yenye lengo la kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa na viwango vizuri katika Bidhaa zake pamoja na  Mazingira mazuri ili kulinda Afya za Binadamu.

"Nilazima Makampuni na Mashirika yanazalisha kwa kutunza Mazingira pamoja na  kujali Afya za Binadamu wanaozunguka katika Kampuni hiyo", Amesema Bw Majengo.

Mgeni Rasmi Katika Semina hiyo Bw, Odila Majengo akiwa kwenye Picha ya Pamoja na wadau mbalimbali waliohudhuria katika Warsha Hiyo.

Mkurugenzi wa Masoko katika Wizara ya Viwanda na Bihashara Bw, Odilo Majengo, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa Warsha hiyo.

No comments:

Post a Comment