KILA
mtu anajua kuwa sheria na haki ni vitu viwili tofauti. Usilazimishe
kupata haki, kwasababu sheria imeonyesha juu ya madai yako. Kufanya hivyo ni kujipotezea muda wako unaoweza kuutumia katika kazi nyingine za maendeleo yako.
Pamoja na yote hayo, lakini wakati mwingine si sahihi kujificha kwenye mhimili wa kisheria kwa kufanya mambo ambayo ni tofauti katika jamii. Kila mmoja anapaswa kuishi kwa upendo bila kuweka u-mimi, vyama vyetu na mengineyo pia.
Nasema haya baada ya Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, maarufu kama ‘Sugu’kutoka (CHADEMA)kuachiwa huru na Mahakama ya Wilaya ya Mkoa wa Dodoma, kwa madai kuwa hati ya mashitaka ina mapungufu kisheria.
Sugu alipandishwa kizimbani katika mahakama hiyo, mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mkoa wa Dodoma, Elinaza Luvanda na kusomewa shitaka linalomkabili kuhusu kutoa lugha ya matusi katika mtandao wa kijamii, moja ya vitu vinavyotumiwa vibaya na watu wengi.
Katika mitandao hiyo, kila mmoja anaandika kile anachojisikia, bila kujali faida au hasara inayopatikana kwa kuandika upupu wake.
Sugu aliandika hivi;”Tanzania haijawahi kupata Waziri Mkuu mpumbavu kama Pinda”.