Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam ameelezea
tukio zima Lililotokea Mbagala na kusema kuwa tukio hilo lilianza juzi octoba
10 ambapo ambapo kijana mwenye miaka
kumi na mbili aliambiwa akikojolea kitabu cha Kuraan utatokewa na nyoka au
madhara mengine yatamtokea.
Amesema kuwa Kijana huyo aliamua kukojolea kitabu hicho
ndipo kijana huyo wa kiislamu ambao wote walikuwa na utani aliamua kwenda
kuwaambia wazazi wake juu ya Tukio zima.
Ndipo wazazi wa huyo kijana wakaamua kukaachini na
kuzungumza ili kumaliza kutokana na kuwa
waliofanya hivyo ni watoto
Kamanda Kova amesema kuwa athari zilizotokea mpaka sasa ni
kwamba tayari waislamu hao wamevunja Makanisa Matatu.
Kamanda ameongeza kuwa hakuna sababu ya kufanya vurugu kwani
hayo ni mambo ya watoto kutokana na kuwa mtoto aliyefanya hivyo ni motto wa
miaka kumi na mbili.
Naye Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik amesema
kuwa anawaomba wakazi wote wa jiji la Dar es Salaam hasa wale waliopo kwenye
eneo la tukio(Mbagala) kuwa wavumilivu ili tatizo hili lililosababishwa na
kijana huyo lisiwe chanzo la uvunjifu wa Amani.
Maswala haya tukianza kuleta chokochoko za imani za kidini mwisho wake huwa unakuwa sio mzuri.
No comments:
Post a Comment