Mabomu ya Machozi yanarindima hivi punde huko mbagala wilayani Temeke ili kuwasambaratisha waislamu waliondamana na kukizunguka kituo cha Polisi Kizuiani wakitaka Polisi imuachie Kijana wa Mkristo wa Kidato cha kwanza aliyekojolea kitabu cha Dini ya kiislamu maarufu kama Msaafu
Kwa taarifa zilizotufikia hivi punde ni kwamba
kijana huyo ambaye jina lake halikuweza kufahamika kwa urahisi ameamua
kufanya hivyo baada ya kutokea Mabishano kati ya yeye na Mwenzie kuwa ukikojolea kitabu hicho utakuwa mwendawazimu ambapo kijana huyo mkristo alipinga na kuamua na kuamua kukojolea Msaafu.
Kijana huyo alikojolea Msaafu ili ahakikishe kuwa kweli atakuwa Mwenda wazimu ama tofauti na baada ya kijana huyo kukojolea kitabu hicho Tukufu ndipo Mwislamu huyo akaamua kuwataarifu waislamu wenzake juu ya Kitendo alichokifanya Mwenzake.
Na mpaka hivi sasa Polisi wameamua kupiga Mabomu ya Machozi ili kuwatawanyisha Waislamu waliokusanyika mahali hapo, ambapo waislamu wengine wanasikika wakisema kuwa ni bora wafie hapo lakini kuondoka hawaondoki.
No comments:
Post a Comment