Fredrick Sumaye akitoa mada kwenye mjadala huo
WAZIRI Mkuu Mstaafu
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Frederick Sumaye, amesema ubinafsi uliopo
kwa baadhi ya viongozi umesasababisha nchi kuingia katika dimbwi la umaskini.
Akiwasilisha mada
kwenye mdahalo wa Maadhimisho ya miaka 13 13 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Juliusi
Nyerere Sumaye alisema viongozi wa sasa wamekuwa wabinafsi kiasi cha kuandaa
watoto na wake zao kwa ajili ya kuwa viongozi wa nchi wa baadaye kama nchi za
kifalme kinyume na katiba ya nchi.
Aliongeza kuwa
ubinafsi huo ndio chanzo kukubwa cha kukithiri kwa rushwa katika sekta
mbalimbali kwa kuwa viongozi hao, hawako tayari kupoteza madaraka yao, badala
yake hutumia rasilimali sambamba na uwezo wao wa kifedha kuwahonga wapiga kura
ili waendelee kukaa madarakani, hata kama wananchi hawawataki.
“Rushwa imekithiri
sehemu muhimu ambazo zingepata viongozi wachache wenye uchu na nchi tusingekuwa
katika eneo hili, Mtu yeyote anayetaka kwenda Ikulu kupitia rushwa hafai’ mosi
hizo fedha za kuwahonga wananchi alipata wapi? Kama amekopa anategemea ikulu
kuna hela ambazo hataweza kurudisha deni hilo?
Aliongeza
“Chaguzi zote
zimetawaliwa na rushwa moja kwa moja jambo ambalo hayati mwalimu Nyerere
halilikemea hadi mwisho wa uhai wake, na kama hatutaliangalia tatizo hilo kwa
makini kuna hadhari kubwa kwa taifa”
“Kila mmoja wetu ajiulize
je angefufuka leo mwalimu Nyerere, nani angeshiriki kumlaki? au angetamani
kuvaa nguo gani ili aonekane kuwa tofauti na mwingine? au tungekuwa wa kwanza
kukimbilia porini? tafadhali
tutafakari na kuchukua hatua ili tuondokane na maovu kwa kuondoa taswira tofauti katika jamii” alisisitiza
Sumaye.
Aidha, alifafanua
kuwa matumizi mabaya ya Ofisi ya Rais ni tatizo kubwa ndani ya nchi kwa sababu
viongozi walioko hawataki kung’oka madarakani badala yake wameng’ang’ania nafasi
hizo kwa maslahi yao ya kuwaandaa watu wao wa baadaye.
Mbali na ubinafsi
huo, aligusia hali ya uchumi wa nchi kukuwa, lakini umeshikiliwa na kundi la watu
wachache, hivyo matukio yanayoonekana kwa sasa ni hatua ya ukiukaji wa sheria
pamoja na amani ya nchi.
“Hali ya kutowajali kundi la watu masikini ni tatizo
kwa taifa, kwa sababu viongozi hao wamewekeza kwa kuwajali wenye nacho ili
wanufaike kama wao, tabia hiyo ni hatari kwa taifa” aliongeza Sumaye.
Naye Mkuu wa Chuo
Dk. John Magotti alitumia fursa hiyo kuzungumzia suala la kiwango cha elimu
itolewayo nchini hususani katika shule za kata kuwa ni chachu ya kukwamisha
ufaulu sanjari na ajira kwa wahitimu.
“Kuna haja ya
serikali kutafuta ufumbuzi katika sekta ya elimu kabla haujaleta madhara
makubwa, kwa sababu elimu bora inaendana na nafasi bora ya ajira, hivyo mwito
wangu elimu inayotolewa katika shule za kata isitofautiane sana na ile ya shule
za watu binafsi” alitabanaisha Magotti.
|
No comments:
Post a Comment