Friday, November 16, 2012

ASKOFU KILAINI AKANA KUIPONDA SAFU YA UONGOZI WA CCM

Kwa masikitiko makubwa nimesoma katika gazeti la Mwananchi kwamba nimeiponda safu ya uongozi na Sekretarieti ya CCM.

Mimi sijaongea na gazeti lolote juu ya uongozi wa CCM na wala sina nia wala sababu ya kuuponda uongozo huo.

Ni vibaya kwa gazeti lo lote lile kutumia jina la mtu kwa kueneza maoni yake. Kama ni waungwana, natumaini watasahihisha waliyoyaandika.

Nasikitika sana kwa waliokwazwa na hilo.

Askofu Method Kilaini.
Bukoba Catholic Diocese.
(anwani pepe imehifadhiwa)

No comments:

Post a Comment