|
Katibu
mkuu ofisi ya waziri mkuu Bw, Peniel Lymo akizungumza katika mkutano
uliowakutanisha wadau mbalimbali wa kupambana na janga la ukimwi ulioandaliwa
na TACAIDS ambapo alisema kuwa wananchi
wanatakiwa kuzingatia ushauri na
kuepukana na vishawishi vibaya vinavyochocea maambukizi ya VVU. |
Amesema kuwa vijana wanatakiwa wahakikishe kuwa janga hili
la ukimwi linaondoka kwani anauhakika kuwa vijana wanaweza kwakuwa wao ndio
kila kitu.
Bw, Lymo alisisitiza
Mashirika yanayojishughulisha na kupambana na Janga la UKIMWI kuhakikisha kuwa pesa zote zitakazotolewa kwa
mashirika mbalimbali kwa ajili ya kusaidia kupunguza janga hili la ukimwi
zitumike sawasawa kwa matumizi ya kuzuia UKIMWI na sio vinginevyo.
|
Katibu
mkuu ofisi ya waziri mkuu Bw, Peniel Lymo
akiwa na Mwenyekiti Mtendaji wa TACAIDS Bi Fatma Mrisho mara baada ya
kuongea na waandishi wa habari katika mkutano huo ambapo Bi Fatuma alisema kuwa
lengo lao kubwa waTACAIDS ni kuhakikisha kuwa UKIMWI unaisha kabisa, kwani
mpaka sasa Takwimu zinaonyesha kuwa watanzania wengi hawajaathirika ambao ni
zaidi ya asilimia 90 hiyo ni kwa maana kwamba ni Watanzania wachache tu ndio
walio athirika. |
|
Baadhi
ya wadau waliohudhuria katika mkutano huo wakisikiliza kwa makini.Mkutano huo
umefanyika leo katika Hoteli ya Bluer Pearl jijini Dar es Salaam. |
No comments:
Post a Comment