Friday, November 9, 2012

MKAKATI WA KUTANGAZA UTALII KIMATAIFA KUZINDULIWA MWEZI HUU

Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akizungumza katika dhifa hiyo kabla ya kukabidhi tuzo kwa makampuni yaliyofanya vizuri katika kuuza na kutangaza utalii wa Tanzania, wa pili kutoka kulia ni Balozi Peter Kallaghe watatu kutoka kulia ni Issa Ahmed Othman Mshauri wa Rais Zanzibar Masuala ya Utalii na kulia ni Bw Yusuf Kashangwa Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza.

Habari na Geofrey Tengeneza --

Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Balozi Khamisi Kagasheki anatarajiwa kuzindua mkakati wa utangazaji utalii wa kimataifa tarehe 15/11/2012 katika hoteli ya Serena hapa jijini Dar es salaam.

Mkakati huo unaotarajiwa kuwa ndio dira ya kuitangaza Tanzania kama eneo la utalii duniani umetengenezwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kwa kushirikiana na Shirikisho la vyama vya Utalii Tanzania (TCT) linajumuisha wadau mbali mbali katika sekta ya utalii hapa nchini.

Hafla hiyo itakayofanyika kuanzia saa 12.30 jioni itahudhuriwa pia na Naibu Waziri Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bibi Maimuna Tarishi, Naibu Katibu Mkuu Bibi Nuru Milao na viongozi wengine kutoka Wizarani. Aidha viongozi wa Shirikisho la vyama vya utalii nchini TCT na wadau wengine wa sekta ya utalii watahudhuria pia hafla hiyo

No comments:

Post a Comment