TANZANIA KUPELEKA MAJESHI DRC
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Bernard Membe, amesema Tanzania iko tayari kupeleka kikosi
cha askari wake 800 kwenda kupambana na waasi wa Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Kongo (DRC), maarufu kama M23.
Ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa haari ambapo amesema kuwa askari hao watajiunga na wengine kutoka nchi za SADC ili wafike 3200 kwa ajili ya jukumu hilo.
Amesema kuwa Wanajeshi hao watasaidia kwenda kulinda mipaka ya DRC na kuzuia baadhi ya miji inayotekwa na waasi wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (M23) ambapo mpaka sasa tayari wameshauteka mji wa Goma.
No comments:
Post a Comment