Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas
Kandoro amewataka waislamu kushirikiana na kujenga umoja miongoni mwao badala
ya kutengeneza majungu ambayo yanaathiri maendeleo yao.
Bw. Kandoro alizungumza hayo
wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Mfuko wa Maendeleo cha mkoa wa Mbeya MRIDEF
kilichopo Sokomatola jijini Mbeya leo asubuhi.
Alisema kuwa waislamu wamekuwa
hawana kawaida ya kujituma katika maendeleo hali ambayo inachangia kwa asilimia
kubwa kurudisha maendeleo hivyo aliwataka kujikita katika kazi katika maeneo
yao ili kuepuka malalamiko ya kutengwa katika shughuli za maendeleo.
'' Jishughulisheni kwenye kazi
za maendeleo na ujasiriamali, tusome elimu zote za dini na dunia, tuwasomeshe
watoto wetu wapate elimu zote za dunia na akhera''alisisitiza Bw. Kandoro.
Alisema kila mzazi aangalie
fursa zinazomzunguka ili ajijengee uchumi katika kaya yake na kumudu huduma za
msingi na kujiongezea kipato halali.
Kwa upande wake Katibu wa mfuko
wa Maendeleo ya Waislamu Mkoa wa Mbeya Shekhe Abbas Mshauri alisema kuwa madhumuni
ya Taasisi hiyo ni kusaidia kuleta maendeleo ya kijamii na kidini na kuongeza
elimu na uchumi wa kila mmoja kulingana na maadili ya Uislamu.
Alisema kuwa taasisi imedhamiria kuweka vitega uchumi na
mahusiano na ushirikiano na asasi zingine za kidini Kitaifa na Kimataifa.
Kwa hisani ya Rashidi Mkwinda
|
No comments:
Post a Comment