Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini
(UNDP) Bw. Phillippe Poinsot akifungua rasmi Siku ya Kimataifa ya
Kujitolea bila malipo kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar
inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 5 Disemba ambapo kauli mbiu ya mwaka
huu ni ‘Volunteer Action Counts’.(Picha na www.dewjiblog.com)
Mgeni
rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kujitolea Mkurugenzi
Msaidizi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo Bi. Venerose
Mtenga akihutubia na kuwaasa vijana kufanya kazi kwa kujitolea bila
kusubiri malipo.
Mgeni
rasmi amewaasa vijana kuwa tayari kufanya kazi kwa kujitolea kwa sababu
Serikali kupitia Wizara yake imetenga Bilioni 1.5 kwenye mfuko Maalaum
wa Vijana ili kuwakopesha vijana kwenye vikundi vidogo vidogo ili
wajiunge na ujasiriamali na kujitoa katika umaskini.
Mshehereshaji
wa Siku ya Kimataifa ya kujitolea Austin Makani akijadiliana na
washiriki kuhusiana na umuhimu wa vijana kujitolea.
Kutoka
kushoto ni Mgeni rasmi Bi. Venerose Mtenga, Mkurugenzi Mkazi wa UNDP
Bw. Phillippe Poinsot na Afisa Program wa Shirika la Umoja wa Mataifa la
kujitole (UNV) Bi. Stella Karegyesa wakifuatilia program zilizokuwa
zikiendelea wakati wa maadhimisho hayo.
Pichani Juu na Chini baadhi ya wanafunzi wa vyuo mbalimbali, wanachama
wa UN Clubs na wageni waalikwa waliohudhuria maadhimisho ya siku ya
Kimataifa ya kujitolea.
Baadhi ya washiriki wakijadiliana umuhimu wa kujitolea katika makundi.
Mgeni rasmi Bi. Venerose Mtenga na Mkurugenzi Mkazi wa UNDP Bw. Phillippe Poinsot wakitoka ukumbi.
Mgeni
rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kujitolea Mkurugenzi
Msaidizi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo Bi. Venerose
Mtenga, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa
nchini (UNDP) Bw. Phillippe Poinsot na Afisa Program wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kujitole (UNV) Bi. Stella Karegyesa katika picha ya pamoja na washiriki.
No comments:
Post a Comment