Monday, December 10, 2012

Rais Kikwete atunuku Nishani Ikulu wakati wa Sherehe za miaka 51 ya Uhuru

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo mchana ametunuku  nishani kwa watu kutoka makundi mbalimbali yajamii waliotumikia taifa kwa uadilifu na kutoa mchango wa pekee.Miongoni wa waliotunukiwa nishani leo ni pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi  Balozi Ombeni Sefue ,Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa Eusebia Munuo pamoja na Msanii Mkongwe Bi.Fatma Baraka Khamis(Bi.Kidude) Pichani juu.Wengine waliotunikiwa nishani ni pamoja na Watumishi wa umma na askari jeshi na polisi(picha na Freddy Maro).
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Bi Fatma Baraka
Khamis,(Kidude) baada ya kutunukiwa nishani ya Sanaa na Michezo na
Rais wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete,(kulia) katika sherehe za
kutunuku Nishani katika Viwanja vya Ikulu Dar es Salaam.[Picha na
Ramadhan Othman,Ikulu.]
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Bi Fatma Baraka
Khamis,(Kidude) baada ya kutunukiwa nishani ya Sanaa na Michezo na
Rais wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete,(kulia) katika sherehe za
kutunuku Nishani katika Viwanja vya Ikulu Dar es Salaam,(katikati)Rais
Mstaafu wa Tanzania Mzee Mwinyi.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

Rais Jakaya Kikwete akimpongeza Jaji Mstaafu Eusebia Munuo akivishwa nishani baada ya kumvisha nishani yake leo



Rais Jakaya Kikwete akimvisha nishani Balozi Ombemi Sefue  ambaye ni  Katibu Mkuu Kiongozi ikulu leo jijini Dar es salaamRais Jakaya Kikwete akimvisha nishani mmoja wa watumishi wa serikali

No comments:

Post a Comment