Thursday, December 20, 2012

MAMLAKA YA HALI YA HEWA WATOA VYETI KWA WAHITIMU WA MAFUNZO YA SIGMENT NA QMS

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini Dkt, Agness Kijazi akitoa Maelezo Mafupi mbele ya Wanafunzi pamoja na Wanahabari waliokuwemo leo wakati wa Hafla fupi ya Ugawaji vyeti  kwa wahitimu wa Mafunzo ya Sgment na QMS  ambapo amesema kuwa pamoja na  Wahitimu kuhitimu  mafunzo hayo wanauwezo wa kutoa ripoti juu ya Hali ya Hewa Mbaya ambapo amesema kuwa Tanzania kuna hali ya Hewa Mbaya hasa katika mko wa Mbeya.
 Dk Kijazi amesema kuwa Wahitimu hao wanauwezo wa kutoa taarifa Sahihi ya hali ya hewa Mbaya kwa Marubani,  jambo ambalo litasaidia kupunguza ajali zinazoweza kutokea Angani. Hafla hiyo imefanyika leo hasubuhi, katika Ukumbi wa mikutano wa Mamlaka hiyo yaliyopo Jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Bw, Morrison Mlaki  akisoma Risala yake mbele ya Wageni walio hudhuria katika Hafla hiyo ambapo Wahitimu walitakiwa kufanya kazi kwa bidii kwa kutoa taarifa sahihi ya hali ya Hewa.

Bw, Morrison Mlaki

Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Bw, Morrison Mlaki akimkabidhi mmoja wa wahitimu cheti chake

Mkurugenzi wa Mamlak ya Hali ya Hewa naye alibahatika kupokea cheti kwa Niaba ya Mamlaka hiyo

Mwenyekiti  wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini  Bw, Morrison Mlaki, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya hewa Nchini Dkt, Agness Kijazi wakiwa kwenye picha ya Pamoja na wahitimu.

No comments:

Post a Comment