Askari
Polisi wakiwa kwenye doria katika eneo la Tukio la Uporaji wa fedha
katika moja ya duka Kariakoo jijini Dar bes salaam mara baada ya uporaji
kufanyika katika eneo hilo.
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum, Seleman Kova akizungumza na waandishi wa habari
katika kituo kikuu car es salaam kuhusiana na tukio hilo.
……………………………………………………
KAMANDA wa Polisi Kanda Maalum,
Seleman Kova amewataka wananchi kuacha kutoa taarifa potofu kuwa baadhi
ya askari walionekana kuchukua mfuko wa fedha katika tukio la wizi wa sh
milioni 150, lilitokea Mtaa wa Mahiwa Kariakoo Dar es Salaam juzi.
Kauli hiyo ya Kova, ambaye pia
ni Naibu Kamishna wa Polisi, imekuja baada mashuhuda wa tukio hilo kudai
kuwa askari waliofika katika eneo la tukio kuonekana wakichukua mfuko
huo uliokuwa umejaa fedha, kutokana kutupwa na jambazi aliyekuwa
akikimbia kwa lengo la kujisalimisha.
Akizungumza na Fullshangweblog janaKova
alisema wakati askari wanamkamata jambazi huyo, kwa bahati mbaya hakuwa
hana mfuko wowote wa fedha kama inavyodaiwa, habari hizo sijui zinatoka
wapi.
Alisema wananchi wanapaswa
kutambuwa kuwa tukio lile linaonekana majambazi wale walilipanga kwa
ustadi hivyo inawezekana wakati anajaribu kujisalimishana alifanikiwa
kulirusha kwenye gari na wenye gari hilo kutoweka nalo.
“Unajua linapotokea tukio kama
hili kila mtu anaweza kusema lake hivyo tunachoweza kueleza ni kuwa
fedha hizo hazijapatikana, tunaendelea na upelelezi na tunahakika
tutawakamata wote waliohusika na tukio lile”alisema Kova.
Akizungumzia madai kuwa askari
walionekana kuchelewa kuwadhibiti majmbazi hao, Kamanda Kova alisema
hawakuchelewa bali wanapofika kwenye matukio ambayo yapo kwenye makundi
ya watu ni lazima watafute engo ya kushambulia kwanza.
Alisema hawawezi kwenda kifua
mbele kwa kushambulia tu kwani wanaweza kuua raia wema, ambapo inaweza
kusababisha malalamiko kutoka kwa raia.
Kuhusu tabia za pikipiki
kuhusishwa kwenye matukio ya ujambazi alisema wataendesha operesheni
kama awali ambapo walizikamata pikipiki 275 kutokana na makosa
mbalimbali ya ukiukaji wa sheria za usalama barabarani, yakiwemo hayo ya
ujambazi.
Juzi majambazi walivamia
wafanyakazi wa Kampuni ya Artan waliokuwa wakijiandaa kupeleka fedha
Benki, tukio lililotokea katika mtaa Mtaa wa Mahiwa Kariakoo jinini
nakusababisha watu wawili kupoteza maisha na wengine watatu kujeruhiwa.
No comments:
Post a Comment