Mbunge
wa Jimbo la Ukonga,Mh. Eugean Mwaiposa (katikati) akizungumza na
Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kwenye ukumbi wa Kimataifa wa
Mikutano wa Dar es Salaam mapema leo asubuhi wakati wa kutangaza
uzinduzi wa Mkakati wake wa kuwainua kiuchumi wananchi wa Jimbo lake la
Ukonga kupitia Mradi aliouanzisha ujulikanao kama “JAMII NA MAENDELEO
UKONGA”,ambapo amefanikiwa kuvikusanya vikundi vya wafanyabiashara ndogo
ndogo waliopo kwenye Jimbo la Ukonga na kwa umoja huo pia ameanzisha
Saccos ya Jimbo itakayowawezesha wafanyabiashara hao kupata mikopo ya
kuendeleza biashara zao inayotambulika kwa jila la UKONGA VICOBA SACCOS
LTD (UVICOSA).Kulia ni Mwenyekiti wa Muda wa Saccos hiyo,Bi. Adivela
Ruge.
Katibu
wa Ukonga Vicoba Sacos (UVICOSA),Bi. Mary Katobes (kushoto) akiongea
wakati wa kuwahamasisha wananchi wa jimbo la Ukonga (kupitia vyombo vya
habari) kujitokeza kwa wingi kujiunga na Sacos yao hiyo.
Meneja wa Mradi wa Jamii na Maendeleo Ukonga,Suzan Miseda akiongea katika mkutano huo na Waandishi wa Habari.
No comments:
Post a Comment