Hii ni moja ya aina za nyumba zinazopatikana katika vijiji vya mkoa wa Dodoma
……………………………………………………………………………
Na. Luppy Kung’alo wa Jeshi la Polisi Dodoma
Mahakama ya Wilaya Kongwa Jana
ilimuhukumu Bw. Jumanne Hassan Miaka (22) ambaye ni mkazi wa kijiji
cha Liganga, Kata ya Chitego tarafa ya Nzoisa wilayani humo kutumikia
kifungo cha miaka (30 ) jela na kuchapwa viboko (12) baada ya kumtia
hatiani kwa kosa la kubaka mwanafunzi wa darasa la tano.
Mwandesha mashtaka Maulid Manu
ambaye ni Mkaguzi wa Polisi (INSPEKTA) aliiambia Mahakama hiyo kuwa
Bw. Jumanne Hassan alimbaka binti mwenye umri wa miaka (12) ambaye
jina lake limehifadhiwa na ni mwanafunzi wa darasa la tano katika
shule ya msingi Liganga iliyopo wilayani kongwa.
Mwendesha mashtaka huyo wa
Polisi, aliieleza mahakama kwamba Bw. Jumanne Hassan alitenda kosa hilo
kwa kumvizia binti huyo aliyekuwa anatoka kununua mahitaji ya dukani
alipokuwa ametumwa kisha kumkamata mkono na kumvutia katika chumba cha
rafiki yake kilichokuwa jirani na eneo hilo kisha kumbaka na
kumtishia kwamba akipiga kelele atamuua.
Alieleza hayo mbele ya mbele ya
hakimu wa mahakama ya Wilaya ya Kongwa Bw. Godfrey Pius, aidha
alisema tukio hilo lilitokea Novemba moja, mwaka jana (2011) majira ya
sa mbili na nusu usiku katika eneo la kijiji cha Liganga, Kata ya
Chitego na Tarafa ya Nzoisa Wilayani Kongwa.
No comments:
Post a Comment