Mgeni
rasmi katika Sherehe za maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu Waziri
Mkuu Mh. Mizengo Pinda akiwasili katika viwanja vya Mnazi Mmoja na
kusalimiana na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa nchini (UNDP) Bw. Phillippe Poinsot.
Pichani
Juu na Chini ni maandamano ya kuadhimisha siku ya Haki za Binadamu
yaliyohusisha Taasisi mbalimbali za Serikali na zisizo za kiserikali,
Wanafunzi wa Shule za Sekondari na Wanaharakati wa Haki za Binadamu
yakiwasili katika Viwanja vya Mnazi Mmoja na kupokelewa na Mh. Waziri
mkuu Mizengo Pinda (hayupo pichani).
Meza
Kuu ikipokea maandamano ya Wanafunzi na Taasisi mbalimbali za
Kiserikali na zisizo za Kiserikali wakati sherehe za maadhimisho ya Siku
ya Haki za Binadamu zilizofanyika jijini Dar leo.
Jaji
Kiongozi (Mstaafu) Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala
Bora Mh.Amiri Ramadhani Manento akisoma hotuba yake katika maadhimisho
ya Siku ya Haki za Binadamu ambapo aliwasilisha Ujumbe wa Katibu Mkuu wa
Umoja wa Mataifa kuwa nchi zote zihakikishe kuwa zinafuata maazimio ya
tamko la haki za binadamu na wananchi wake wanufaike na haki zilizomo
ndani yake.
Mwanasheria Mkuu wa Sreikali Jaji Frederick Werema akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Haki za Binadamu.
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP) Bw.
Phillippe Poinsot akizungumza kwa niaba ya Mratibu Mkazi wa Umoja wa
Mataifa ambapo amesema chini ya mpango wa pamoja, Umoja wa Mataifa
nchini Tanzania unasaidia vitengo muhimu vya serikali na wadau wengine
wa mzunguko wa Haki za Binadamu, kwa mfano ofisi ya Mwanasheria Mkuu,
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na idadi kubwa ya Asasi zisizo
za kiserikali zinazohusika na masuala ya Haki za Binadamu.
Vilevile
amesema Umoja wa Mataifa unaendelea kuinga mkono serikali kufuatilia
ahadi zilizotolewa kwa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa na
mapendekezo yakiwemo kutoka katika Bodi za Mikataba ya haki za
Binadamu.
Afisa Mipango kutoka Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu Kanda
ya Afrika Mashariki Bw. Abdu Mohammed akisoma hotuba kwa niaba ya
Kamishna wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa ambapo amesisitiza kila
raia anapaswa kuwa na haki na fursa ya kushiriki katika masuala ya
umma, moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi huru wa kuchaguliwa, pia
kila binadamu ana haki ya kupiga kura na kuchaguli na na kuweza kufikia
huduma za kijamii sambamba uhuru wa kujieleza, kukusanyika na kuungana.
Amongeza
kuwa haki hizi zinatakiwa kumhusu kila mtu na hakuna hata mmoja atakaye
baguliwa kwa moja kati ya hizo kwa sababu ni mwanamke, au anatoka
katika kundi dogo, au anaabudu katika dini Fulani, au kwa sababu ni
shoga, au ana ulemavu, anaamini siasa Fulani, au mkimbizi au ana rangi
fulani, anatoka katika kabila Fulani.
Mgeni
rasmi Mh. Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisoma hotuba yake ambapo amesema
Pamoja na kuadhimisha kumbukumbu ya Siku ya Haki za Binadamu, pia
tunaadhimisha kumbukumbu ya Siku ya Kimataifa ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa kwa pamoja. Kaulimbiu ya mwaka huu katika Kupambana na Rushwa ni
“Unaweza kuzuia rushwa, chukua hatua sasa”. Kauli hii inaonesha umuhimu
wa Wananchi wa rika zote kupiga vita rushwa.
Mh.
Pinda amesema hatua ya kuunganisha maadhimisho haya na kufanyika sehemu
moja kunapunguza gharama kwa upande wa Serikali, na pia kunatoa nafasi
kwa Wananchi kufahamu umuhimu wa siku zote mbili bila kulazimika
kuondoka eneo moja la tukio kwenda eneo jingine. Napenda kuzipongeza
Taasisi zote husika kwa kuunganisha matukio haya mawili na kuadhimisha
sehemu moja na kwa wakati mmoja.
Ameongeza
kuwa Huu ni mwaka wa tano tangu Taifa letu lilipoanza kuadhimisha siku
hii Kitaifa. Kaulimbiu ya Kimataifa kwa mwaka huu ni: “Sauti yangu
inachangia” (My voice counts). Ujumbe huu unatukumbusha kushiriki katika
kutoa maoni katika shughuli mbalimbali za Kijamii au Kitaifa.
Mh. Waziri mkuu Mizengo Pinda akizindua taarifa ya miaka 10 ya Tume ya
Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB). Wanaoshuhudia uzinduzi huo ni
Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Mathias Chikawe (kushoto) na Naibu wake
Mh. Angellah Kairuki (kulia).
Sasa
imezinduliwa rasmi….Mh. Waziri mkuu Pinda akionyesha ripoti hiyo kwa
wageni waalikwa (hawapo pichani). Kulia ni Jaji Kiongozi (Mstaafu)
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mh.Amiri
Ramadhani Manento na Kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Mathias
Chikawe (kushoto).
Waziri Mkuu Pinda akipitia ripoti hiyo.
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP) Bw.
Phillippe Poinsot akipitia nakala taarifa ya miaka 10 ya Tume ya Haki za
Binadamu na Utawala Bora.
Kikundi
cha Wana wandime ya kwetu ngoma wakitoa burudani wakati wa sherehe za
maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu yaliyofanyika katika viwanja vya
Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.
Pichani
Juu na Chini ni Wafanyakazi wa Taasisi mbalimbali za Serikali na zisizo
za serikali, Wanafunzi wa shule za Sekondari, Wadau wa Haki za Binadamu
na Wananchi wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Haki za
Binadamu.
Mgeni rasmi Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika picha ya pamoja na Viongozi
wa Tume ya Haki za Binadamu na Waziri wa Katiba na Sheria na Naibu
wake.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiagana na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mh. Mahfoudha Alley Hamid.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiondoka katika viwanja vya Mnazi Mmoja baada
ya sherehe za maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu huku
akisindikizwa na Mkurugenzi Mkazi wa UNDP, Naibu Waziri wa Katiba na
Sheria na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
No comments:
Post a Comment