Uongozi
wa Skylight Entertainment na Skylight Band, unatoa tamko la kulaani
kitendo cha watu wachache waovu wenye tabia ya kuvuruga Amani kwenye
sehemu za burudani. Tunapenda kuwahikikishia wapenda burudani wa jiji la
Dar es Salaam kuwa tutaendelea kutoa burudani mpya na inayokidhi kiu
cha muda mrefu cha wapenda burudani katika fani ya muziki wa live.
Aidha
tunakemea vitendo vyovyote vya ubabe wa kizamani usio na tija kwa
jamii. Tunaamini maeneo ya burudani ni kwaajili ya kukutana, kuburudika,
kufahamiana, kuondokana msongo wa mawazo unaotokana na maisha ya kila
siku na kutengeneza network na watu mbalimbali kijamii, kikazi na
kibinafsi. Eneo la burudani sio kwaajili ya kuonesha wengine wewe ni
nani na una uwezo gani. Tunawaomba wana burudani wote tushirikiane
pamoja kuwakemea na kuwafichua, kulaani na kuwatenga wote wanaoashiria
vitendo vya uvunjifu wa amani. Tunaendelea kuimarisha ulinzi na
kuwahakikishia burudani kwa kwenda mbele.
Karibu
Thai Village kila ijumaa ujumuike na marafiki na kupata burudani na
ladha za kimataifa. Tunawashukuru wapenzi na washabiki wa Skylight kwa
kutupokea vizuri ndani ya muda mfupi.
Mungu ibariki Skylight, Mungu Ibariki Tanzania.
Imetolewa na
Mkurugenzi Mtendaji
Skylight Entertainment.
No comments:
Post a Comment