Wanachama
wa UWF (Unity of Women Friends) wakiwa katika picha ya pamoja mara
baada ya kumaliza matembezi yao hisani ya kilometa tano kwa ajili ya
kuchangisha fedha za kuwasomesha watoto wa kike wa shule ya Tandika na
Tabata sekondari ambao wanaishi kwenye mazingira magumu na wengi wao
wanatoka kwenye familia duni,matembezi hayo yamefanyika mwishoni mwa
wiki huku mgeni rasmi akiwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la
HakiElimu,Bi.Elizabeth Missokia (wa tatu kutoka kulia)..
Wanachama
wa UWF (Unity of Women Friends) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi
ya wanafunzi wa shule ya Tandika na Tabata sekondari
Mgeni rasmi,Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la HakiElimu,Bi.Elizabeth Missokia akizungumza machache wakati wa hafla fupi ya kuchangisha
fedha za kuwasomesha watoto wa kike wa shule ya Tandika na Tabata
sekondari ambao wanaishi kwenye mazingira magumu na wengi wao wanatoka
kwenye familia duni,Bi Elizabeth kupitia shirika hilo la HakiElimu
waliahidi kutoa shilingi milioni tatu ikiwa sehemu ya mchango wao
kuhakikisha watoto wa kike wanapata elimu.
Mwenyekiti wa UWF
(Unity of Women Friends),Esther Wakati akifafanua madhumuni/lengo la
matembezi hayo ya hisani kwa mgeni rasmi na wageni waalikwa
wengine,Easther alisema kuwa lengo la matembezi hayo ni kuchangisha
shilingi milioni 80,ambazo zitasaidia kusomesha wanafunzi 100,Tandika
wanafunzi 50 na Tabata wanafuzi 50 kwa kipindi cha miaka 4.
Mweka hazina wa UWF
(Unity of Women Friends),Bi.Mwate Mwadinda akitoa makusanyo
yaliyopatikana kwenye matembezi hayo ya hisani ya Kilometa tano,Mwate
alisema kuwa hafla yao imefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi milioni
kumi na laki mbili,hiyo ikiwa ni hatua ya awali ya muendelezo wa
kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasomesha watoto wa kike ambao wanaishi kwenye mazingira magumu na wengi wao wanatoka kwenye familia duni
Meneja
Mradi wa SOMKI (Somesha Mtoto wa Kike),Bi Jane Magembe akizungumza
machache mbele mgeni rasmi na wageni waalikwa mbalimbali waliofika
kwenye hafla hiyo fupi,kuhusiana mradi/mfuko wa SOMKI unatumika
kuwasomesha watoto wa kike waishio katika mazingira magumu,Mradi huo uko
chini ya UWF.
Baadhi
ya wanafunzi wanaosomeshwa na mfuko wa SOMKI,kutoka kulia ni Khadija
Hassan Chizenga anaesoma kidato cha nne shule ya Sekomdari Kunduchi
Girls High School pamoja na Ummilkhery Abdallah anaesoma kidato cha sita
shule ya sekondari Benjamin William Mkapa high school.
Wanachama wa UWF wakifurahi jambo.
Baadhi
ya wageni waalikwa waliofika kwenye hafla hiyo fupi iliyofanyika ndani
ya Police Oficcers Mess,Oysterbay,jijini Dar mwishoni mwa wiki.
Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,aitwae Vumi akiimba kwa hisia mbele ya wageni waalikwa.
Pichani
juu na chini ni wanachama wa UWF wakiwa na mgeni rasmi sambamba na
wageni waalikwa wakiwa kwenye matembezi ya hisani ya kilometa
tano,yakiwa na lengo ya kuchangisha
shilingi milioni 80,ambazo zitasaidia kusomesha wanafunzi 100,Tandika
wanafunzi 50 na Tabata wanafuzi 50 kwa kipindi cha miaka 4.Matembezi
hayo yalidhaminiwa na taasisi ya Foundation for Civil Society,kampuni ya
Clouds Media gROUP,Securix,ITRATECH LTD,Prime Time Promotions,Cool Blue
pamoja na Equip Davith Kahwa.
No comments:
Post a Comment