Na Heka Wanna na Shakila Galus,MAELEZO
MWENYEKITI wa WAMA Mama Salma
Kikwete wito kwa wananchi tabia ya kujisomea vitambu na machapisho
mbalimbali ili kujiongezea maarifa yatakayowawezesha kujiletea
maendeleo.
Mama Kikwete alitoa kauli hiyo
kwenye Makumbusho ya Taifa leo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi
wa makatba kwa ajili ya watoto na watu wazima.
Alisema kuwa elimu ndio silaha
pekee ya kukabiliana na maadui watu ambao ni ujinga,maradhi na umaskini
na hivyo kujiletea maendeleo.
Mama Kikwete aliongezea mbinu za
kujiendeleza kimaisha zinapatikana pia kwa njia elimu kupitia vitabu na
machapisho mbalimbali yanayopatikana kwenye maktaba mbalimbali ndani na
nje ya Tanzania.
Alisema kuwa hiyo itasaidia
katika kuongeza maarifa kwani kutakuwa na vitabu,kompyuta na mitambo ya
mawasiliano ambayo itawawezesha watumiaji kupata elimu ya taaluma
mbalimbali.
Aidha Mama Kikwete aliwasihi
watumishi wa Makumbusho hiyo kuwa ni jukumu lao kutunza maktaba hiyo ili
isaidie kukidhi malengo ya kuanzishwa kwake kwa kuandaa taratibu bora
za kudhibiti matumizi yasiyo na tija ya maktaba ikiwemo upotevu
machapisho na vitabu mbalimbali na uhalibifu wa vitabu unaofanywa na
watu wasiotaka maendeleo.
Mwenyekiti huyo WAMA alimshukru
Balozi wa Korea Kusini Young Shimo Dho kwa niaba ya nchi yake kwa
msaada wa vitabu na vifaa mbalimbali kwa ajili ya maktaba hizo mbili .
No comments:
Post a Comment