Saturday, December 22, 2012

OMBAOMBA 14 KURUDISHWA MAKWAO


OMBAOMBA1 4 watasafirishwa makwao baada ya kukamatwa ndani ya Kituo cha Mabasi yaendayo mikoani na Nje ya nchi , Ubungo (UBT), wakiishi kama makazi yao ya kudumu kinyume cha sheria.
 Akizungumza na Fullshangweblog  jijini Dar es Salaam leo, Meneja wa Kituo hicho Juma Iddi, alisema ombaomba hao walikamatwa wiki moja iliyopita na kufikishwa katika Mahaka ya jiji.
Alisema uwamuzi wa kuwasafirish watu hao umetokana na hukumu iliyotolewa na Mahaka kutokana na kuwabaini kuwa walikuwa na makosa, hata hivyo, kutokana na hali zao  iliamuru warudishwe makwao ikiwa ndiyo adhabu yao.
Iddi alisema watu hao watarudishwa nyumbani kwao kwa kulipiwa nauli na Mamlaka ya jiji, ambapo watakaporudi tena Malaka hiyo haitawasamehe.
“Mikakati yetu ni kuondoa kero zote kwa abiria wetu, angali ombaomba hawa baadhi yao ni wakorofi na wamekuwa wakiishi humu miongoni mwao wakifanya  ngono hadharani kwa makusudi sasa hali kama hii haikubaliki katika jamii”alisema Iddi.
Vilevile alisema operesheni hiyo ni endelevu na  hawatorudi nyuma bali wanawatahadharisha wale wote wanaoendesha shughuli zao bila ya kufuata sheria watambuwe kuwa wakati wao wakuchukuliwa hatua za kisheria umefika.
Iddi alibainisha kuwa opersheni inaenda kwa awamu ambapo ya kwanza imejihusisha na kuwaondoa ombaomba inayofuata itawahusu wapiga debe, wachafuzi wa mazingira, vibaka na kundi la watoto ambalo linaonekana kuongezeka katika kituo hicho.
Hata hivyo, operesheni hiyo ili iweze kuzaa matunda bado ushiriki wa wadau wa kutoa taarifa kwa wasimamizi wa kituo hicho unahitajika

No comments:

Post a Comment