Friday, January 18, 2013

AJARIBU KUJILIPUA KWA PETROL AKIWA NJE YA KITUO KIDOGO CHA POLISI RUNGWE MBEYA

RPC  MBEYA KAMANDA DIWANI


MNAMO TAREHE 17.01.2013 MAJIRA YA SAA 23:00HRS HUKO KATIKA ENEO LA KIWIRA KATA YA KIWIRA WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA. JOSEPH S/O MWAENGA, MIAKA 32, KYUSA, MWENDESHA PIKIPIKI @ BODABODA NA MKAZI WA KIWIRA. ALIJIMWAGIA MWILINI MAFUTA AINA YA PETROLI NA KISHA KUMWAGIA MAFUTA MENGINE KITUO KIDOGO CHA POLISI KIWIRA NA KUTOA KIBERITI KWA NIA YA KUTAKA KUJILIPUA. MTUHUMIWA ALIDHIBITIWA NA ASKARI WALIOKUWA ZAMU KWA KUMKAMATA NA KUMUWEKA CHINI YA ULINZI. HAKUNA MADHARA YA KIBINADAMU WALA MALI YALIYOTOKEA. CHANZO CHA TUKIO HILI NI MTUHUMIWA KUFANYA FUJO  KATIKA KIJIWE/KITUO CHAKE CHA BODABODA AKIWA AMELEWA NA ALIPOTAKA KUKAMATWA  NA WANANCHI ALIKIMBIA HIVYO WANANCHI KUICHUKUA PIKIPIKI YAKE NA KUISALIMISHA KITUO CHA POLISI KIWIRA NDIPO MTUHUMIWA ALIKWENDA KITUO CHA POLISI AKIWA BADO AMELEWA HUKU AKIWA NA DUMU LA MAFUTA YA PETROLI. TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI MTUHUMIWA AFIKISHWE MAHAKAMANI.  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUTOKUTUMIA VILEVI KUPITA KIASI KWANI INAWEZA  KUSABABISHA MADHARA  MAKUBWA PASIPO KUTARAJIA.
Signed By,
[DIWANI ATHUMANI – ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments:

Post a Comment