CHAMA cha Wananchi (CUF) Wilaya ya Handeni, mkoani Tanga
kimewatahadharisha wananchi kuepuka kuwaunga mkono watu au viongozi
wanaohamahama na kuanzisha vyama vya siasa, kikidai wanataka kujinufaisha
binafsi.
Acheni kuwaunga mkono watu wanaoanzisha vyama vipya, haiwezekani kwa mfano mtu umekaa CUF karibu miaka 20, leo unaanzisha chama kipya eti unahimiza watu wakufuate, haiwezekani,” alisema Katibu wa CUF Wilaya ya Handeni, Masoud Mjaila na kuongeza: “Kwani hao watu umewachukua ‘msukule’ wakufuate kila unakotaka kwenda… Hapana, wakataeni.”
Mjaila alikuwa akihutubia mkutano wa hadhara wilayani hapa juzi, uliokuwa ukilenga kuweka mambo sawa, baada ya wiki iliyopita Chama cha ADC kukishambulia kwa kukituhumu kuanzisha migodi ya madini wilayani humo isiyokuwa na kibali. Katika mkutano huo, Mjaila alikiri wana kampuni inayomiliki migodi minane ya madini mbalimbali Kijiji cha Sezakofi, Kata ya Ndolwa.
Alisema wanaimiliki kihalali huku akionyesha vibali, hatua iliyolenga kujaribu kujisafisha, kufuatia kurushiwa tuhuma na Mlezi wa ADC Kanda ya Kaskazini, Hassan Doyo, aliyejiunga na chama hicho baada ya kutimuliwa CUF.
“Wananchi msikubali kuburuzwa, hiki chama chenu cha CUF kina miaka 20 tangu kuanzishwa, hapa Handeni kina miaka 15, lakini mnaona hali ilivyo, ndiyo hivi karibuni sasa na sisi tupo ndani ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa,” alisema Mjaila na kuongeza: “Sasa hawa ADC wameanza jana, leo wanataka waungwe mkono, hapana! Hawa wanatafuta masilahi yao maana huku CUF walifukuzwa. Eti wanasema migodi ile ya madini haina vibali, siyo kweli kwani serikali iko wapi, tumechangia zaidi ya milioni 3.5/= kusaidia miradi mbalimbali ya Serikali ya Kijiji cha Sezakofi.”
Alisema wanatambua vijembe hivyo vinatokana na fitina zilizojaa viongozi wa ADC, hawataki CUF wapate maendeleo.
Aliwashauri nao kutumia fursa zilizopo kwa ajili ya kujipatia maendeleo badala ya malumbano majukwaani.
Katika mkutano huo, CUF kilitangaza kutoa msaada wa shuka 20 zenye thamani ya Sh180,000 hospitali ya wilaya hiyo. Pia, walitoa sabuni zenye thamani ya Sh150,000.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa chama hicho wilayani hapa, Jumaa Magogo, alisema wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo wanauziwa uji. Magogo alisema kitendo hicho siyo cha kiungwana na kwamba, kinafanywa na mawakala waliopewa kazi ya kutoa huduma hiyo na halmashauri ya wilaya.
---
via gazeti la MWANANCHI

No comments:
Post a Comment