Wednesday, January 16, 2013

Boni Yayi (Rais Benin MKiti AU) afanya mazungumzo na Rais Kikwete nchini Tanzania

 
Picture
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akimlaki kwa furaha Rais wa Benin na Mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika, Mhe. Thomas Boni Yayi mara baada ya Rais huyo kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam tarehe 15 Januari 2013 kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
Rais wa Benin ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (UA), Mhe. Boni Yayi aliwasili hapa nchini tarehe 15 Januari, 2013 saa 2.00 usiku kwa ziara ya kikazi ya siku moja.

Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Mhe. Yayi allipokelewa na Mwenyeji wake Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akiwa nchini Mhe. Yayi alifanya mazungumzo usiku na mwenyeji wake Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Ikulu, Dar es Salaam. Mbali na kuzungumzia masuala ya ushirikiano kuhusu nchi hizi mbili, viongozi hao wamezungumzia masuala muhimu kuhusu Bara la Afrika.

Mhe. Yayi alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika wakati wa Mkutano wa 18 wa Wakuu wa Nchi wa Umoja huo uliofanyika Addis Ababa, Ethiopia mwezi Januari 2012 na atamaliza muda wake wa uenyekiti wakati wa Mkutano wa 20 wa Wakuu wa Nchi wa Umoja huo utakaofanyika pia Addis Ababa tarehe 27 na 28 Januari 2013.

Mhe. Yayi anaondoka tarehe 16 Januari 2013.
Picture
Mhe. Rais Yayi akisalimiana na Viongozi mbalimbali wa Serikali waliofika kumlaki alipowasili nchini. Pichani Rais Yayi akisalimiana na Balozi Vincent Kibwana, Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Picture
Kikundi cha Burudani kilichofika Uwanjani hapo wakati wa mapokezi ya Mhe. Rais Yayi.

No comments:

Post a Comment