NA MOBINI SARYA,TANPRESS
WAKATI juhudi za kusafisha mitaa
ya katikati ya jiji la Dar es Salaam,zikiwa zimeshika kasi kampuni ya
kufua umeme Tanesco imelaumiwa kukwamisha juhudi hizo kwa kukata miti na
kuacha taka zimezagaa hivyo.
Akizungumza na shirika la habari
nchini Tanpress msemaji wa kampuni ya Green Weste Pro Ltd iliyopewa
tenda ya kuzoa taka maeneo ya kati kati ya Jiji,Vidah Joseph alisema
kuwa wamejitahidi kuzoa uchafu kwa masaa 24 lakini wanasikitishwa na
kitendo cha Tanesco kukata miti na kuacha taka hovyo.
Bi. Joseph alisema kuwa Shirika
la umeme Tanesco limekuwa likikata Miti inayoegemea nguzo za umeme bila
kuitaarifu kampuni ya kuzoa taka jambo linalosababisha majani ya miti
hiyo kugeuka takataka.
“Mkataba wetu ni kuzoa taka za
majumbani sio kuzoa miti inayokatwa barabarani, halafu sasa bora hawa
Tanesco wangekuwa wanatupa taarifa kabla ili sisi tujiandae kuzoa
lakini wanakata miti hovyo wanaacha taka huku sisi hatuna taarifa
tukiwafuata wanatuambia wametoa tenda ya kukata miti tukiwauliza
watuambie aliyekata miti hawasemi”anasema Bi Joseph
Jana Kampuni hiyo ambayo inajukumu
la kuzoa taka Kata ya Kivukoni, Mchafukoge na Kisutu,ililazimika
kuwaita wandishi wa habari waende kujionea taka za miti zilizozagaa
kwenye mitaa ya umoja wa mataifa na Palm city na katikati ya jiji baada
ya wafanyakazi wa yanesco kukata miti kisha kuondoka bila kuzoa majani.
Kutokana na kitendo hicho Kampuni
ya Green Weste ilisema kuwa tanesco wanapaswa kuzoa au kulipia taka
hizo ili mkandarasi azizoe kwasababu hata wale wanaojenga barabara na
majengo wakimwaga michanga na kifusi hulipia wanapohitaji kuzolewa.
Msemaji wa Tanesco,Badra Masoud
alipotafutwa, simu yake iliita bila kupokelewa hadi tunakwenda mitamboni
ingawa viongozi wa Weste Pro waliahidi kulifikisha suala hilo
halmashauri, ili kampeni yao ya safisha jiji kwa masaa 24 isikwmaishwe.
No comments:
Post a Comment