Kamati ya Utendaji ya
Shirikisho la Kimataifa la wahandisi Washauri (FIDIC) linatarajia kufanya
mkutano wake wa siku mbili jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam
Mjumbe wa FIDIC Eng, Exaud Mushi amesema kuwa Mkutano huo
utafanyika tarehe 23 na 24 mwezi huu katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaa.
Eng, Mushi amesema kuwa ni mara ya kwanza kwa FIDIC kufanya
mkutano huo nchini Tanzania tangu shirikisho hilo liundwe miaka 99 iliyopita.
Rais wa ACET Eng Menye Manga amesema kuwa, Miongoni mwa
wajumbe watakao kuwepo kwenye Mkutano huo ni pamoja na Rais wa FIDIC kutoka Uingereza, Makamu wa rais mteule (Spain)
pamoja na wajumbe wengine saba wanaotoka Canada, Ufaransa, Sweden, Tanzania,
Jordan, Korea ya kusini na Japan.
Rais wa ACET pamoja na Mjumbe wa Bodi ya FIDIC katika mkutano wa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam |
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria kwenye Mkutano huo |
No comments:
Post a Comment