Mkuu
wa Jeshi la Polisi Nchini Said Mwema akimkabidhi pikipiki Kamanda wa
Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam, Naibu Kamishna wa Polisi Suleiman
Kova kama ishara ya kukabidhiwa Makamanda wote Tanzania bara na
Visiwani ambapo jumla ya Pikipiki 564 zimekabidhiwa kwa ajili ya kuzuia
uhalifu kwa lengo la matumizi ya Wakaguzi Tarafa wa Polisi Tanzania bara
na Majimbo yote ya Zanzibar, program za Safiri Salama na Usalama wetu
kwanza.
Makabidhiano hayo yamefanyika
katika makao makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es salaam na
kuhudhuriwa na Makamanda na maafisa mbalimbali wa jeshi hilo.
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam, Naibu Kamishna wa Polisi
Suleiman Kovaakijaribhu mkuwasha moja ya pikipiki zilizotolewa kwa
maofisa mbalimbali wa jeshi hilo nch nzima mara baada ya makabidhiano
anayeangalia katikati na Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Said Mwema
na kulia ni Mkurugenzi wa Benki ya Posta Bw. Sabasaba
Afande Inspekta Mkweru akijaribu moja ya pikipiki zilizokabidhiwa leo kwa maafisa wa jeshi hilo.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini IGP Said Mwema kulia akiwa katika hafla ya
makabidhiano hayo makao makuu ya jeshi la polisi jijini Dar es salaam
leo asubuhi, katikati ni Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Polisi Paul Chagonja na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam, Naibu Kamishna wa Polisi Suleiman Kova
Maafisa mbalimbali wa jeshi la polisi wakiwa katika hafla hiyo leo asubuhi.
Maafisa mbalimbali wa jeshi la polisi wakiwa katika hafla hiyo leo asubuhi.
Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Polisi Paul Chagonjaakizungumza jambo na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania Advera Senso wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya pikipiki zilizokabidhiwa kwa maafisa hao wa polisi leo
No comments:
Post a Comment