WAKATI
Serikali na Bunge zikiwa kwenye mvutano kuhusu hatua za kufuatwa kurejesha
mabilioni ya fedha za Kitanzania yaliyofichwa kwenye benki za nchini Uswisi,
swali kubwa lililopo ni kwamba ni akina hasa ambao wana fedha huko.
Mtoaji wa hoja binafsi kuhusu suala hilo, Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA),
Zitto Kabwe, amegoma kutaja majina ya vigogo wanaotajwa kuhifadhi fedha akitaka
uchunguzi ufanyike na majina yafahamike wakati huo, huku serikali ikimtaka
ataje majina ili ipate pa kuanzia kwenye uchunguzi huo.
Serikali kupitia Mwanasheria Mkuu, Jaji Frederick Werema, inataka kuendesha
uchunguzi kuhusu madai hayo ya Zitto lakini kwanza inataka mbunge huyo ataje
majina ya baadhi tu ya vigogo ambao ana ushahidi wamehifadhi fedha Uswisi.
Pamoja na hayo, swali moja ni lazima lipate majibu, leo au kesho. Swali lenyewe
ni hili; ni akina nani waliokwiba fedha za Watanzania na kwenda kuzihifadhi
ughaibuni?
Niseme mapema kwamba kuwa na akaunti nje ya nchi si dhambi. Dhambi inakuja pale
inapofahamika kwamba fedha hizo zilipatikana isivyo halali.
No comments:
Post a Comment